// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 18, 2016

    SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    SIMBA SC imeondoka Morogoro baada ya mazoezi ya leo jioni kurejea Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu, Yanga SC.
    Watani hao wa jadi, wanatarajiwa kumenyana keshokutwa katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huo ukiwa mchezo wa marudiano, baada ya mchezo wa kwanza Septemba mwaka jana, Yanga kushinda 2-0.
    Simba SC iliweka kambi Morogoro tangu Jumatatu baada ya kushinda michezo miwili mfululizo mjini Shinyanga dhidi ya Kagera Sugar 1-0 na dhidi ya Stand United 2-1 Uwanja wa Kambarage.

    Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kufikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambako wachezaji watapumzika kabla ya mchezo wa Jumamosi.
    Wapinzani wao, wako Pemba tangu Jumapili baada ya kuwasili Mauritius, ambako walishinda 1-0 dhidi ya wenyeji Cerle de Joachim katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Na Yanga pia wanatarajiwa kuwasili kesho mchana Dar es Salaam, wao pia wakiwa na mpango wa kufikia katika hoteli moja ya nyota tano katikati ya Jiji. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WATUA DAR USIKU TAYARI ‘KUTAFUNA KANDAMBILI’ JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top