Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm (kushoto) amesema kwamba mechi na Cercle de Joachim leo haitakuwa nyepesi
Kiungo mahiri wa Yanga, Thabani Kamusoko |
Mholanzi huyo amesema kwamba hakuna mechi nyepesi na timu ndogo kwenye michuano yoyote ya soka, hivyo jioni ya leo Uwanja wa Taoifa, Dar es Salaam na atashusha 'kikosi cha maana' kusaka ushindi wa pili dhidi ya timu hiyo ambayo haipewi nafasi kubwa ya kusonga mbele.
"Haitakuwa mechi nyepesi, kila timu inataka kufanya vizuri ili kusonga mbele," Pluijm aliwaambia waandishi wa habari. "Tutaingia na kasi ya kushambulia ili kutafuta magoli, sipendi mfumo wa kulinda lango."
Yanga leo itahitaji hata sare ya aina yoyote ili kusonga mbele Raundi ya kwanza ya michuano hiyo, baada ya awali kushinda 1-0 Mauritius.
Na mabingwa hao wa Bara, watawakosa viungo Haruna Niyonzima na Salum Telela, ambao ni majeruhi, wakati mshambuliaji tegemeo, Donald Ngoma amekwenda kwao, Zimbabwe jana baada ya kufiwa na mdogo wake.
Yanga watamenyana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland katika Raundi ya Pili.
0 comments:
Post a Comment