UHONDO wa Ligi ya mabingwa Ulaya unaanza rasmi leo, wakati mechi mbili zitakapopigwa kwenye viwanja tofauti, ukiwa huku mchezo gumzo zaidi ukiwa kati ya Arsenal na mabingwa watetezi, Barcelona.
Arsene Wenger anaikaribisha timu ya Luis Enrique leo Saa 4:45 usiku wa leo Uwanja wa Emirates London, katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 16 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
Homa kubwa kwa Arsenal washambuliaji watatu hatari wa Barca, Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar ambao kwa pamoja 'MSN' wamefunga mabao 91 msimu.
Wachezaji wa Arsenal wakijifua kuelekea mchezo na Barcelona leo Uwanja wa Emirates |
Kwa Arsenal, wakali wa kutegemewa ni Olivier Giroud, Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao kwa pamoja wamefunga mabao 34 msimu huu.
Barcelona, mabingwa mara tano wa Ulaya, walioifunga Juventus ya kocha Massimiliano Allegri mabao 3-1 Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin, Ujerumani Juni mwaka jana kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa kwa ujumla wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi zote, Emirates na Camp Nou.
Timu ya mwisho kuizuia Barcelona kufunga bao katika mechi, ilikuwa Espanyol katika mechi ya wapinzani wa Katalunya Uwanja wa Power8 Januari 2 mwaka huu walipotoa sare ya 0-0 na tangu wakati huo, Barca imefunga mabao 46.
Wakali wa mabao wa Barcelona; Messi kulia na Suarez na Neymar kushoto wakijadiliana mazoezini |
Mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo ni kati ya washindi wa pili wa mwaka jana Juventus dhidi ya FC Bayern Munich Uwanja wa Juventus, wakati kesho Dynamo Kyiv wataikaribisha Manchester City Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev na PSV watakuwa wenyeji wa Atletico Madrid Uwanja wa Philips.
0 comments:
Post a Comment