// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSWISI AWA RAIS WA TISA FIFA, NI MWANASHERIA NA KATIBU WA ZAMANI UEFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSWISI AWA RAIS WA TISA FIFA, NI MWANASHERIA NA KATIBU WA ZAMANI UEFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 26, 2016

    MSWISI AWA RAIS WA TISA FIFA, NI MWANASHERIA NA KATIBU WA ZAMANI UEFA

    Katibu Mkuu wa zamani wa UEFA, Gianni Infantino amekuwa Rais mpya wa FIFA, baada ya kumshinda Sheik Salman  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    RODHA YA MARAIS WA FIFA 

    1904-06: Robert Guerin (Ufaransa)
    1906-18: Daniel Woolfall (England)
    1918-21: no president in place following Woolfall's death
    1921-54: Jules Rimet (Ufaransa)
    1954-55: Rodolphe Seeldrayer (Ubelgiji)
    1955-61: Arthur Drewry (England)
    1961-74: Sir Stanley Rous (England)
    1974-98: Joao Havelange (Brazil)
    1998-2015: Sepp Blatter (Uswisi)
    2016-present: Gianni Infantino (Uswisi)
    MSWISI mwenye asili ya Italia, Gianni Infantino amekuwa Rais wa tisa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mjini Zurich, Uswisi leo na akaahidi kurejesha hadhi ya soka uliwenguni katika zama mpya.
    Kura za uchaguzi wa FIFA leo zimepigwa mara mbili kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 42 baada ya Infantino, Katibu wa zamani wa UEFA kutomshinda kwa nusu ya kura mpinzani wake wa karibu, Sheik Salman bin Ibrahim al Khalifa wa Bahrain katika Raundi ya kwanza.
    Katika kura za raundi ya pili zilizohusisha wapinzani hao wawili tu, Infantino alikusanya 115 huku Sheik Salman, akipata 88 na kuwa Mswisi wa pili mfululizo kukamata Urais wa FIFA, baada ya Sepp Blatter.
    Mwanasjeria huyo kitaaluma mwenye umri wa miaka 45 anatokea Brig mjini Valais, Uswisi, kiasi cha maili sita kutoka nyumbani kwao Blatter, Visp.
    Blatter alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 na akaendelea kushinda chaguzi tano zilizofuata, ukiwemo wa Mei mwaka jana, lakini akalazimika kujiuzulu siku kadhaa baadaye kufuatia tuhuma na ukosefu wa maadili zilizoambatana na kufungiwa miaka sita kujihusisha na masuala ya soka, ambayo ameendelea kujihusisha nayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSWISI AWA RAIS WA TISA FIFA, NI MWANASHERIA NA KATIBU WA ZAMANI UEFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top