// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MPINZANI WA CHEKA KUWASILI DAR JUMATANO, NAPE MGENI RASMI LEADERS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MPINZANI WA CHEKA KUWASILI DAR JUMATANO, NAPE MGENI RASMI LEADERS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 19, 2016

    MPINZANI WA CHEKA KUWASILI DAR JUMATANO, NAPE MGENI RASMI LEADERS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BONDIA Mserbia, Gerad Ajetovic anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumatano ijayo kwa ajili ya pambano la ngumi za kulipwa dhidi ya Mtanzania, Francis Cheka Februari 27, mwaka huu kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF.
    Meneja wa Cheka, Juma Ndambile ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo mjini Dar es Salaam kwamba, Rais wa WBF, Goldberg Haward na timu yake wasimamizi wa pambano hilo wanatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi.
    Ndambile pia amesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni katika pambano hilo la raundi 12, uzito wa Super Middle litakalofanyika viwanja vya Leaders, Kinondoni mjini Dar es Salaam.

    Bondia Gerad Ajetovic anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumatano tayari pambano na Francis Cheka Februari 27 

    Ndambile, amesema maandalizi yote yamekamilika na Waziri Nape amekubali ombi la kuwa mgeni katika pambano hilo, ambalo litatanguliwa na mapambano kadhaa, ikiwemo burudani ya bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'.
    "Napenda pia kuwaambia mashabiki wa ngumu kuwa Cheka yuko fiti na kusisitiza kwamba hajawahi kuwaangusha Watanzania akiwa hapa nyumbani," alisema.
    Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mabondia hapo kupigana baada ya mwaka 2008 kuzidunda nchini England na Cheka kupigwa kwa pointi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MPINZANI WA CHEKA KUWASILI DAR JUMATANO, NAPE MGENI RASMI LEADERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top