// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKUDE AOMBA MSHIKAMANO SIMBA SC, ASEMA LIGI BADO HAINA MWENYEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKUDE AOMBA MSHIKAMANO SIMBA SC, ASEMA LIGI BADO HAINA MWENYEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, February 26, 2016

    MKUDE AOMBA MSHIKAMANO SIMBA SC, ASEMA LIGI BADO HAINA MWENYEWE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA Nahodha wa Simba SC katika mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga SC mwishoni mwa wiki, Jonas Gerald Mkude ameomba wanachama na wapenzi waendelee kuisapoti timu ili itimize malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE baada ya kupoteza mchezo wa watani kwa kufungwa 2-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mkude amesema kwamba wamesikitishwa mno na matokeo hayo, lakini wanapswa kusimama imara na kusonga mbele.
    Jonas Mkude ameomba mshikamano Simba SC 

    “Kama ilivyo kaulimbiu yetu Simba, Nguvu Moja, sasa tutawekeza nguvu zetu kwenye michezo inayofuata na ni matumaini yetu bado wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba tutakuwa pamoja katika kuendelea kuhakikisha kuwa ubingwa msimu huu unakuja Msimbazi,” amesema.
    Simba SC ilipokonywa usukani wa Ligi Kuu baada ya kuchapwa 2-0 watani wao, Yanga mabao ya Mzimbabwe Donald Ngoma kipindi cha kwanza na Mrundi Amissi Tambwe kipindi cha pili.
    Matokeo yaliifanya Yanga ifikishe pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda kileleni, wakati Simba SC iliyocheza mechi 20, inaporomoka hadi nafasi ya tatu ikibaki na pointi zake 45, sawa na Azam FC nayopanda nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao (GD).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUDE AOMBA MSHIKAMANO SIMBA SC, ASEMA LIGI BADO HAINA MWENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top