// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAYANJA AWAPANGIA VIUNGO KIBAO YANGA, WASHAMBULIAJI WALE WALE, KIIZA NA HAJIB - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAYANJA AWAPANGIA VIUNGO KIBAO YANGA, WASHAMBULIAJI WALE WALE, KIIZA NA HAJIB - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 20, 2016

    MAYANJA AWAPANGIA VIUNGO KIBAO YANGA, WASHAMBULIAJI WALE WALE, KIIZA NA HAJIB

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Simba SC, Jackson Mayanja amepanga kikosi kilichotarajiwa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
    Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Uganda na klabu za KCCA na SC Villa za kwao, amepanga viungo wengi, akiweka washambuliaji wawili tu, Mganda mwenzake Hamisi Kiiza na mzalendo, Ibrahim Hajib.
    Mayanja, kocha wa zamani wa Kagera Sugar na Coastal Union amewapanga viungi Mzimbabwe Justice Majabvi na wazalendo Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla katika mchezo huo, wakati safu ya ulinzi inaundwa na kipa Vicent Angban raia wa Ivory Coast, mabeki wa pembeni Hassan Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na wa katikati Juuko Murshid na Abdi Banda.
    Hiki ni kikosi cha Simba SC kilichoanza Septemba 26, mwaka jana Yanga ikishinda 2-1   

    Kikosi cha Simba SC kinachoanza leo ni; Vicent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Abdi Banda, Justice Majabvi, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Hamisi Kiiza, Ibrahim Hajib na  Said Ndemla,
    Benchi; Peter Manyika, Novatus Lufunga, Hassan Isihaka, Danny Lyanga, Mussa Mgosi na Brian Majwega.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYANJA AWAPANGIA VIUNGO KIBAO YANGA, WASHAMBULIAJI WALE WALE, KIIZA NA HAJIB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top