// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
KAVUMBANGU ANUSURIKA KIFO CHA AJALI DAR, GARI YAKE ‘NYANG’ANYANG’A’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEKAVUMBANGU ANUSURIKA KIFO CHA AJALI DAR, GARI YAKE ‘NYANG’ANYANG’A’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
KAVUMBANGU ANUSURIKA KIFO CHA AJALI DAR, GARI YAKE ‘NYANG’ANYANG’A’
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu, anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, leo amenusurika katika ajali mbaya, lakini gari yake aina ya Toyota Premio ‘halitamaniki’. Kavumbangu ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati anatoka nyumbani kwake, Kijichi kwenda hospitali ya Dk Gilbert, Mikocheni kwa matibabu ya majeruhi yake yanayomuweka nje tangu mwezi uliopita.
Gari ya Didier Kabumbangu (picha ndogo kulia) inavyoonekana kwa mbele baada ya ajali
Mipira ya kumzuia aliye ndani ya gari asiumie ikiwa imechomoka kutokana na ajali hiyo
Amesema wakati anakata kona kwenye mzunguko wa magari yanayotoka Kijichi na Mbagala kuelekea mjini, ndipo alipogongwa na gari kubwa la mizigo, ambalo ‘limeiharibu sura’ gari yake kwa mbele. “Kisheria inatakiwa wale wanaotoka Mbagala watusubiri sisi tunaozunguka tupite, lakini jamaa hakusimama akapita na moto akaipitia gari yangu kwa mbele yote imeharibika sura,”amesema.
Didier Kavumbangu amekuwa nje tangu mwezi uliopita kutokana na majeruhi
Na Kavumbangu anasikitika jamaa baada ya kugonga hakusimama akakimbia na hakukuwa na trafiki karibu wa kuja japo kupima ajali. “Kwa kuwa mimi sikuumia, nikaona hapa nitapoteza muda bure, nikaita gari la kuvuta gari yangu, mimi nikaenda zangu kwa Dokta Gilbert,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
Toyota Premio ya Kavumbangu inavyoonekana kikamilifu baada ya ajali leo
Uganda U17 Boys Face Kenya in Group A Finale
-
The Uganda U17 Boys National Team is bracing for one of the most pivotal
matches in their campaign as they take on familiar rivals Kenya in the
final Gro...
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment