FURAHA YA KABILA DRC KUBEBA CHAN 2016, AWAZAWADIA MAGARI WACHEZAJI
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila ametimiza ahadi yake kwa kumpa kila mchezaji wa timu ya taifa gari kila moja baada ya kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee. DRC walitwaa Kombe hilo Jumapili kwa kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda na leo wachezaji wote walialikwa Ikulu mjini Kinshasa kwa pongezi na zawadi zao za magari.
Wachezaji wa DRC wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Kabila leo Ikulu mjini Kinshasa
Gari aina ya Jeep zikiwa viwanja vya Ikulu mjini Kinshasa leo
Benchi la Ufundi na wachezaji wote, kila mmoja ana Jeep lake moja
DRC ambao walipewa dola za Kimarekani 750,000 kwa kutwaa Kombe hilo, huku Mali wakipata dola 400,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. Ivory Coast waliomaliza nafasi ya tatu na Guinea wa nne, kila timu imepata dola 250,000 walifurahi pamoja na Rais wao leo. Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
Afcon Preview: Nigeria host Rwanda
-
Having sealed their Africa Cup of Nations involvement, Nigeria host
Rwanda in Monday’s final qualifying game at Godswill Akpabio Stadium,
aiming to en...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment