Bondia Francis Cheka wa Tanzania, (kulia) akizuia makonde ya mpinzani wake, Geard Ajetovic Muingereza mwenye asili ya Serbia katika pambano lao la raundi 12 kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super Middle usiku wa kuamkia leo viwanja vya Leaders Club, Kinondoni mjini Dar es Salaam. Cheka alishinda kwa pointi. PICHA ZOTE NA MUHIDDIN SUFIANI WA MAFOTO BLOG
Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake....
Cheka alichanika juu ya jicho la kushoto katika raundi ya nane, lakini akasimama imara na kumaliza pambano
Cheka akiwa amemtandika ngumi ya mbavuni mpinzani wake
Cheka akimtupia ngumi mfululizo za kumchagua Geard Ajevotic
Cheka alikuwa katkika wakati mgumu jana mbele ya Mserbia huyo anayeshi Uingereza
Cheka akiinuliwa mkono kutangazwa mshindi baada ya raundi ya 12
Hapa tayari amevalishwa mkanda wake wa ubingwa wa Mabara wa WBF
Bondia Cossmas Cheka akivalishwa mkanda wa ubingwa wa WBF Afrika uzito wa Light baada ya kumshinda Mtanzania mwenzake, Mustafa Dotto katika pambano la raundi 12Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akimpiga ngumi ya kidevu mpinzani wake, Bakari Mohamed katika pambano lisilo la ubingwa raundi sita uzito wa Light. Matumla alishinda kwa pointi
0 comments:
Post a Comment