MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England mwezi Januari.
Mkali huyo wa mabao wa Argentina ameisaidia sana The Blues ya Manchester kutofungwa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Aguero amefunga jumla ya mabao saba Januari na kutoa pasi moja ya bao, The Blues ikikusanya pointi nane katika mechi nne.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alifunga la ushindi dakika za lala salama City ikianza kampeni ya mwezi huo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford lakini The Blues wakalazimishwa sare ya bila mabao na nyumbani na Everton katika mchezo uliofuata.
Aguero akaifungia mabao mawili timu ya Manual Pellegrini ikiibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Crystal Palace kabla ya kufunga mawili mengine katika sare ya 2-2 na West Ham na akaisaidia pia City kuifunga Everton katika mechi mbili za Kombe la Ligi na kutinga fainali, ambako watakutana na Liverpool Uwanja wa Wembley.
REKODI YA AGUERO JANUARY ENGLAND
2 - vs Watford (bao 1 ushindi wa 2-1)
16 - vs Crystal Palace (mabao 2 ushindi wa 4-0)
23 - vs West Ham (mabao 2 sare hya 2-2)
Ronald Koeman ameshinda tuzo ya kocha Bora wa Mwezi Januari England
Kwa kutwaa tuzo ya Januari, Aguero amewapiku mshambuliaji wa Liverpool, Firmino, kipa wa Leicester, Kasper Schmeichel, beki wa Southampton, Virgil van Dijk, mshambuliaji wa Sunderland, Jermain Defoe na kiungo wa Tottenham, Dele Alli aliokuwa anachuana nao.
Naye Ronald Koeman ameshinda tuzo ya kocha Bora wa Mwezi Januari England, baada ya kuiongoza Southampton kuzifunga Watford, West Brom na Manchester United.
MAKOCHA BORA WA MWEZI MSIMU HUU ENGLAND
AGOSTI; Manuel Pellegrini (Manchester City)
SEPTEMBA; Mauricio Pochettino (Tottenham Hotspur)
OKTOBA; Arsene Wenger (Arsenal)
NOVEMBA; Claudio Ranieri (Leicester City)
DESEMBA; Quique Sanchez Flores (Watford)
JANUARI; Roanald Koeman (Southampton)
0 comments:
Post a Comment