MATOKEO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA…
Januari 21, 2016
Yanga SC 5-0 Majimaji
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
African Sports 0-0 Mtibwa Sugar
Januari 20, 2016
JKT Ruvu 0-2 Simba SC
Mgambo JKT 1-2 Azam FC
Stand United 2-1 Toto Africans
Ndanda FC 3-1 Mbeya City
Prisons 2-1 Coastal Union
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerudi tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji ya Songea jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 39, sawa na Azam FC wanaorudi nafasi ya pili – na vijana wa kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm wanakaa juu kwa wastani mzuri wa mabao.
Mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe amefunga mabao matatu leo, wakati Wazimbabwe, kiungo Donald Ngoma na mshambuliaji Thabani Kamusoko wamefunga bao moja kila mmoja.
Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, dalili za Yanga kuwafanya ‘vibaya’ Majimaji zilianza mapema tu dakika ya nne, baada ya Kamusoko kufunga bao la kwanza akimalizia krosi ya kiungo Deus Kaseke.
Baada ya bao hilo, pamoja na Yanga SC kuendelea kuwashambulia Majimaji, lakini hawakufanikiwa kuongeza mabao hadi kipindi cha pili.
Ngoma alifunga bao la pili dakika 47 kabla ya Tambwe kufunga mara tatu mfululizo dakika za 57, 82 na 84 kuunenepesha ushindi wa mabingwa hao watetezi.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imeshinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na African Sports imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mechi za jana Simba SC iliifunga JKT Ruvu 2-0, Azam FC iliilaza 2-1 Mgambo JKT, Stand United iliichapa 2-1 Toto Africans, Ndanda FC iliikung’uta 4-1 Mbeya City na Prisons ilishinsa 2-1 dhidi ya Coastal Union.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma dk22, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Salum Telela, Simon Msuva/Issoufou Boubacar dk67, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Paul Nonga dk78, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
Majimaji: David Burhani, Alex Kondo, Bahati Yusuph, Mpoki Mwakinyuke, Sadiq Gawaza, Lulanga Mapunda/Kennedy Kipepe dk33, Peter Mapunda/Hassan Hamisi dk63, Paul Maona/Godfrey Taita dk70, Marcel Bonaventura, Sixmund Mwakasega na Frank Sekule.
Januari 21, 2016
Yanga SC 5-0 Majimaji
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
African Sports 0-0 Mtibwa Sugar
Januari 20, 2016
JKT Ruvu 0-2 Simba SC
Mgambo JKT 1-2 Azam FC
Stand United 2-1 Toto Africans
Ndanda FC 3-1 Mbeya City
Prisons 2-1 Coastal Union
![]() |
Refa John Fanuel wa Shinyanga akimkabidhi mpira Amissi Tambwe baada ya mechi kwa kufunga hat trick |
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerudi tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji ya Songea jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 39, sawa na Azam FC wanaorudi nafasi ya pili – na vijana wa kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm wanakaa juu kwa wastani mzuri wa mabao.
Mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe amefunga mabao matatu leo, wakati Wazimbabwe, kiungo Donald Ngoma na mshambuliaji Thabani Kamusoko wamefunga bao moja kila mmoja.
Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, dalili za Yanga kuwafanya ‘vibaya’ Majimaji zilianza mapema tu dakika ya nne, baada ya Kamusoko kufunga bao la kwanza akimalizia krosi ya kiungo Deus Kaseke.
Baada ya bao hilo, pamoja na Yanga SC kuendelea kuwashambulia Majimaji, lakini hawakufanikiwa kuongeza mabao hadi kipindi cha pili.
Ngoma alifunga bao la pili dakika 47 kabla ya Tambwe kufunga mara tatu mfululizo dakika za 57, 82 na 84 kuunenepesha ushindi wa mabingwa hao watetezi.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imeshinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na African Sports imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mechi za jana Simba SC iliifunga JKT Ruvu 2-0, Azam FC iliilaza 2-1 Mgambo JKT, Stand United iliichapa 2-1 Toto Africans, Ndanda FC iliikung’uta 4-1 Mbeya City na Prisons ilishinsa 2-1 dhidi ya Coastal Union.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma dk22, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Salum Telela, Simon Msuva/Issoufou Boubacar dk67, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Paul Nonga dk78, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
Majimaji: David Burhani, Alex Kondo, Bahati Yusuph, Mpoki Mwakinyuke, Sadiq Gawaza, Lulanga Mapunda/Kennedy Kipepe dk33, Peter Mapunda/Hassan Hamisi dk63, Paul Maona/Godfrey Taita dk70, Marcel Bonaventura, Sixmund Mwakasega na Frank Sekule.
0 comments:
Post a Comment