// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YAANZA NA MOTO, YAITANDIKA 3-0 MAFUNZO, NGOMA APIGA MBILI, MOJA NONGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YAANZA NA MOTO, YAITANDIKA 3-0 MAFUNZO, NGOMA APIGA MBILI, MOJA NONGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, January 03, 2016

    YANGA SC YAANZA NA MOTO, YAITANDIKA 3-0 MAFUNZO, NGOMA APIGA MBILI, MOJA NONGA

    MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI 2016
    Kundi A: Simba SC, Jamhuri, JKU, URA
    Kundi B: Yanga SC, Mafunzo, Azam FC, Mtibwa Sugar
    (Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

    Jan 3, 2016
    Yanga SC 3-0 Mafunzo
    Mtibwa Sugar Vs Azam FC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 4, 2016
    JKU Vs URA (Saa 10:15 jioni)
    Simba SC Vs Jamhuri Saa 2:15 usiku)
    Jan 5, 2016
    Mafunzo Vs Mtibwa Sugar (Saa 10:15 jioni)
    Azam FC Vs Yanga SC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 6, 2016
    Jamhuri Vs JKU (Saa 10:15 jioni)
    URA Vs Simba SC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 7, 2016
    Azam Vs Mafunzo (Saa 10:15 jioni)
    Mtibwa Sugar Vs Yanga (Saa 2:15 usiku)
    Jan 8, 2016
    Jamhuri Vs URA (Saa 10:15 jioni)
    Simba SC Vs JKU (Saa 2:15 usiku)
    NUSU FAINALI
    Jan 10, 2016
    FAINALI
    Jan 13, 2016 (Saa 2:15 usiku)
    Thabani Kamusoko (kulia) akimpongeza Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma baada ya kufunga

    Na Princess Asia, ZANZIBAR
    YANGA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuichapa Mafunzo FC mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Mshambuliaji Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na mshambuliaji mpya, Paul Nonga akaingia mwishoni mwa kipindi cha pili na kufunga bao katika mpira wa kwanza kugusa.
    Mafunzo waliuanza vizuri mchezo wa leo na dakika ya kwanza tu mshambuliaji wake Sadikc Habib alikaribia kufunga kama si shuti lake kuokolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’.
    Ngoma akaifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya 31 akimalizia krosi ya Mzimbabwe mwenzake, Thabani Scara Kamusoko aliyemtoka vizuri beki wa Mafunzo kulia. 
    Dakika mbili baadaye, Ngoma tena akafunga bao akimalizia pasi ya Kamusoko tena, aliyemtoka beki upande wa kulia wa boksi na hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0. 
    Kipindi cha pili, Yanga SC walianza kucheza kwa kuwadharau wapinzani, hivyo kuwasogeza kwenye eneo lao na dakika ya 81 Mafunzo wakapoteza nafasi nzuri ya kupata bao, baada ya Dida kupangua mkwaju wa penalti wa Kheri Salum. Penalti hiyo ilitolewa na Refa Mfaume Ali baada ya Shaaban Ali kukwatuliwa na beki wa Yanga SC, Kelvin Yondani ndani ya boksi.
    Paul Nonga aliyeingia dakika ya 88, aliifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 89 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Khalid Mahadhi, kufuatia shuti la Godfrey Mwashiuya aliyeingia pia dakika za lala salama.
    Mchezo wa pili wa Kundi B utafuatia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Amaan, Azam FC wakimenyana na Mtibwa Sugar, wakati kesho kutakuwa na mechi za Kundi A, kati ya JKU na URA Saa 10:15 jioni na Simba SC, mabingwa watetezi dhidi ya Jamhuri Saa 2:15 usiku.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani, Simon Msuva/Malimi Busungu dk88, Thabani Kamusoko/Jerome Sina dk70, Amissi Tambwe/Paul Nonga dk88, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Geofrey Mwashiuya dk70.
    Mafunzo FC: Khalid Mahadhi, Juma Mmanga, Samih Nuhu/Haji Ramadhani dk58, Kheri Salum, Hassan Juma/Haji Abdi dk66, Abdul Hassan, Ali Juma/Jermaine Seif dk72, Sadick Habib/Shaaban Ali dk58, Mohammed Abdul na Ali Mmanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAANZA NA MOTO, YAITANDIKA 3-0 MAFUNZO, NGOMA APIGA MBILI, MOJA NONGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top