![]() |
Chris Katongo (juu) ameifungia bao pekee Zambia ikiilaza Uganda 1-0 na kutinga Robo Fainali CHAN |
Bao lililoizamisha The Cranes leo limefungwa na mkongwe, Christopher Katongo dakika ya 41, akimalizia kazi nzuri ya Benson Sakala.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Mali imeweka hai matumaini ya kusonga mbele baada ya kuilaza 1-0 Zimbabwe, bao pekee la Moussa Sissoko dakika ya 82.
Zambia sasa inafuzu Robo Fainali kwa ushindi huo, wakati The Cranes itatakiwa kushinda dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa mwisho na kuimba Zambia iifunge Mali, ili Korongo wa Kampala wafuzu Robo Fainali kama washindi wa pili.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za Kundi A, wenyeji Rwanda wakimenyana na Morocco na Ivory Coast wakimaliza na Gabon.
0 comments:
Post a Comment