// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA: SITAKI MATATIZO NA MAZEMBE WALA MOISE KATUMBI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA: SITAKI MATATIZO NA MAZEMBE WALA MOISE KATUMBI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 29, 2016

    SAMATTA: SITAKI MATATIZO NA MAZEMBE WALA MOISE KATUMBI

    Na Mwandishi Wetu, GENK
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema hataki matatizo na klabu yake ya zamani, TP Mazembe na anaomba wafikie mwafaka na klabu yake mpya, KRC Genk. 
    Samatta ameyasema hayo leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Genk wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na klabu ya Koninklijke Racing Club Genk kwa Mkataba wa miaka minne na nusu.
    Samatta amesema Mazembe ilimchukua akiwa kijana mdogo na anaishukuru kwa kumlea vizuri na kukuza kipaji chake hadi kutimiza ndoto ya kucheza Ulaya.
    Mbwana Samatta akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Genk leo

    “Wakati ukiwa na ndoto, na unahisi ndoto zako zipo katika njia hii, na nini kinatokea, ni kama kuna kiza mbele yako, lakini naiheshimu Mazembe, namuheshimu Moise (Katumbi), Rais wa Mazembe na sitaki matatizo yoyote na wao,”. 
    “Kwa sababu walinichukua mimi nikiwa bado mdogo mno, nimekulia pale, hivyo nasubiri wakati mwafaka, klabu zifikie makubaliano,”amesema.
    Mwanasoka huyo Bora Anayecheza Afrika. 
    Hatimaye KRC Genk imetimiza ndoto za kumpata mshambuliaji bora, Samatta aliyewasili jana Brussels na moja kwa moja kusafiri hadi Genk.
    Samatta aliyezaliwa Desemba 23, mwaka 1992, anaondoka Mazembe baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, ubingwa wa Ligi Kuu ya DRC mara nne na Super Cup ya DRC mara mbili.
    Samatta aliyejiunga na Mazembe ya Lubumbashi, DRC mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu msimu baada ya kujiunga nayo kutoka African Lyon, zamani Mbagala Market, Mkataba wake na KRC Genk unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020.

    ANGALIA VIDEO SAMATTA AKIZUNGUMZA KIMOMBO GENK
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA: SITAKI MATATIZO NA MAZEMBE WALA MOISE KATUMBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top