// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MECHI MBILI ZA AZAM ‘ZATIWA KAPUNI’, SIMBA NA YANGA WANA KAZI NA WANATANGA J’MOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MECHI MBILI ZA AZAM ‘ZATIWA KAPUNI’, SIMBA NA YANGA WANA KAZI NA WANATANGA J’MOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, January 25, 2016

    MECHI MBILI ZA AZAM ‘ZATIWA KAPUNI’, SIMBA NA YANGA WANA KAZI NA WANATANGA J’MOSI

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Januari 30, 2016
    Coastal Union Vs Yanga SC
    Simba SC Vs African Sports
    JKT Ruvu Vs Majimaji
    TZ Prisons Vs Azam FC
    Mtibwa Sugar Vs Stand United
    Mwadui FC Vs Toto Africans
    Kagera Sugar Vs Mbeya City
    Januari 31, 2016
    Mgambo JKT Vs Ndanda FC
    Mechi mbili za Azam FC zimefutwa ili waende Zambia kwenye michuano maalum
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MECHI mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za Azam FC zimefutwa na zitapangiwa tarehe nyingine ya kufanyika.
    Mechi hizo ni dhidi ya Prisons uliokuwa ufanyike Uwanja wa Sokoine, Mbeya Jumamosi wiki na dhidi ya Stand United uliopangwa kufanyika Februari 3, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Hiyo inafuatia Azam FC kusafiri leo kwenda Zambia kushiriki michuano maalum na inatarajiwa kurejea Februari 4, mwaka huu.
    Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba wamepata ruhusa maalum kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya ziara yao na mechi zao hizo mbili za Ligi Kuu zitapangiwa tarehe nyingine.

    Kawemba amesema kwamba watakaporejea Februari 4, wataendelea na ratiba watakayoikuta ya Ligi Kuu, kuanzia mchezo na Mwadui FC Februari 7, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
    Na Kawemba ameema mechi zao za viporo zitachomekwa katikati ya ratiba yao kuanzia hapo kulingana na nafasi ambayo itaonekana inafaa kwao na kwa wapinzani wao.
    Azam FC imealikwa nchini Zambia kushiriki michuano maalumu inayoshirikisha timu nne, iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa klabu mbili za huko, Zesco United na Zanaco FC.
    Michuano hiyo itaanza keshokutwa Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola na mbali na Azam FC, Zesco na Zanaco, timu nyingine itakayoshirki mabingwa wa Ligi Kuu Zimbabwe, Chicken Inn.
    Pamoja na Azam FC kwenda Zambia, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea Jumamosi, Coastal Union wakiikaribisha Yanga SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Simba SC wakiwa wenyeji wa African Sports wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mechi nyingine ni kati ya JKT Ruvu na Majimaji Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Mwadui FC na Toto Africans Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mwinyi, Tabora. 
    Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu, kati ya Mgambo JKT na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI MBILI ZA AZAM ‘ZATIWA KAPUNI’, SIMBA NA YANGA WANA KAZI NA WANATANGA J’MOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top