Kipre ameinusuru Azam kuzama kwa Zesco |
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye mvua, Zesco walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Jesse Were dakika ya kwanza tu.
Azam FC ilisota hadi mwishoni mwa kipindi cha pili ilipofanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 90.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Waziri Salum/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk67, David Mwantika, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao/Kipre Balou dk46, Frank Domayo, John Bocco/Allan Wanga dk67 na Kipre Tchetche.
Mchezo mwingine wa michuano hiyo, wenyeji wengine Zanaco wamelazimishwa sare ya 2-2 Chicken ya Zimbabwe.
Zanaco ilipata mabao yake kupitia kwa Roderick Kabwe na Fashion Sakala, wakati ya Chicken Inn yalifungwa na Brian Juru na Obidiah Tarumbwa.
Zesco itacheza na Zanaco kesho, wakati Azam itacheza na Chicken Inn.
0 comments:
Post a Comment