Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hata yeye na uzee wake na kitambi chake, lakini akikutana na mabeki kama wa jana wa Majimaji iliyocheza na Yanga SC atafunga hat trick, tena mbili.
Yanga SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Amissi Tambwe alifunga mabao matatu peke yake.
Na Hans Poppe amesema mabeki wa Majimaji jana waliwatengenezea mazingira wachezaji wa Yanga kufunga mabao rahisi – kiasi kwamba anaamini hata kama yeye angekuwapo uwanjani angefunga.
“Pamoja na uzee wangu huu na kitambi changu, kama nikikutana na mabeki kama hawa wa Majimaji, ninafunga hat trick, tena mbili,”amesema.
Poppe amefurahishwa mno na bao la nne la Yanga SC lililofungwa na Tambwe, baada ya beki wa Majimaji, Sadiq Gawaza kuanguka mbele ya Tambwe aliyeupitia mpira na kwenda kufunga.
Ushindi huo wa jana unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 39, sawa na Azam FC wanaorudi nafasi ya pili – na vijana wa kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm wanakaa juu kwa wastani mzuri wa mabao.
Mbali na Mrundi, Tambwe amefunga kupiga hat trick, Wazimbabwe, kiungo Donald Ngoma na mshambuliaji Thabani Kamusoko kila mmoja alifunga bao moja.

Hans Poppe ameubeza ushindi wa Yanga SC jana dhidi ya Majimaji |

Mabeki wa Majimaji wakimsindikiza Tambwe kufunga jana Uwanja wa Taifa |
0 comments:
Post a Comment