JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekata tiketi ya kwenda Nusu Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Rwanda.
Ulikuwa mchezo mgumu na wa kusisimua uliodumu kwa dakika 120, baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
Hatimaye Botuli Padou Bompunga akaibuka shujaa wa DRC kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 114 na ‘kuwaliza’ maelfu ya Wanyarwanda waliojitokeza kwa wingi Uwanja wa Amahoro kuishangilia Amavubi.
DRC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Doxa Gikanji dakika ya 11, kabla ya Ernest Sugira kuisawazishia Rwanda dakika ya 56 akimalizia pasi ya Jean Claude Iranzi.
Robo Fainali ya pili inafuatia sasa kati ya Cameroon na Ivory Coast Uwanja wa Huye mjini Butare.
Kikosi cha Rwanda kilikuwa; Ndayishimiye Eric, Nshimiyimana Amran, Mukunzi Yannick, Bayisenge Emery, Jacques Tuyisenge, Iranzi Jean Claude, Omborenga Fitina, Ndayishimiye Celestin, Sugira Ernest, Habyarimana Innocent/ Dominique Savio Nshuti dk83 na Rwatubyaye Abdul/Dany Usengimana dk83.
DRC; Ley Matampi, Joyce Lomalisa, Padou Bompunga, Mechak Elia/Zacharie Mombo dk93, Doxa Gikanji, Heritier Luvumbu, Nelson Munganga/Ricky Tulengi dk108, Merveille Bope, Joel Kimwaki, Jonathan Bolingi Mpangi na Yannick Bangala.

0 comments:
Post a Comment