BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic atasaini Mkataba wake mpya wiki hii baada ya kukubali kuongeza mwaka mmoja zaidi wa kuendelea kuwajibika Stamford Bridge.
Mkongwe huyo wa umri wa miaka 31, hivi karibuni alipewa ofa ya Mkataba mpya na The Blues ili kuwakatisha tamaa Manchester City, AC Milan, Inter na Zenit St Petersburg wanaomtaka.
Ivanovic, ambaye amecheza mechi 22 za mashindano yote kwa Chelsea msimu huu, anatarajiwa kumaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu na kwa sasa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine.
Branislav Ivanovic anatarajiwa kuongeza Mkataba mpya wa mwaka mmoja Chelsea licha ya kutakiwa na mahasimu, Manchester City pia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment