MABEKI WA KIGENI NA MABAO YAO TIMU ZA BARA:
Beki Timu Mabao Mechi
Serge Wawa Azam FC 0 56
Juuko Murushid Simba SC 2 41
Vincent Bossou Yanga SC 1 10
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
BEKI Mtogo wa Yanga SC, Vincent Bossou amecheza mechi 10 tu hadi sasa tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwanzoni mwa msimu, lakini tayari amefunga bao moja.
Maana yake, Bossou amempiku beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal wa Azam FC, ambaye yuko katika msimu wa pili Tanzania Bara akiwa amecheza mechi 56, lakini hana bao.
Bossou aliyefunga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Azam FC mechi ya Kundi B Kombe la Mapinduzi katikati ya wiki baada ya kutokea benchi kipindi cha pili, sasa anaanza kuifukuzia rekodi ya beki Mganda wa Simba SC, Juuko Murushid.
Juuko aliye katika msimu wa pili pia Bara, hadi sasa amecheza mechi 41 na kufunga mabao mawili Msimbazi.
Tofauti ya Juuko na Wawa, walioanza mara moja kucheza baada ya kusajiliwa, Bossou alilazimika kusubiri hadi Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aumie Novemba mwaka jana ili kuanza kucheza.
Ilifikia wakati hadi waandishi na wachambuzi wa vyombo vya habari wakaanza kuamini Yanga SC imesajili mchezaji galasa, kutokana na Bossou kutopangwa – lakini baada ya kuanza kucheza amebadilisha upepo.
Sasa wana Yanga SC wanamkubali Bossou kama beki wa kazi ambaye anazimudu hata mechi zinazochafuka, kama ile dhidi ya Azam FC iliyotawaliwa na undava.
Sasa wana Yanga wanapenda Bossou apangwe kila mechi ngumu, baada ya shughuli alioionyesha ndani ya mechi 10 tu za mwanzo.
Beki Timu Mabao Mechi
Serge Wawa Azam FC 0 56
Juuko Murushid Simba SC 2 41
Vincent Bossou Yanga SC 1 10
Beki Mtogo wa Yanga SC, Vincent Bossou amewasuta waliokuwa wanaamini yeye galasa |
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
BEKI Mtogo wa Yanga SC, Vincent Bossou amecheza mechi 10 tu hadi sasa tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwanzoni mwa msimu, lakini tayari amefunga bao moja.
Maana yake, Bossou amempiku beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal wa Azam FC, ambaye yuko katika msimu wa pili Tanzania Bara akiwa amecheza mechi 56, lakini hana bao.
Bossou aliyefunga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Azam FC mechi ya Kundi B Kombe la Mapinduzi katikati ya wiki baada ya kutokea benchi kipindi cha pili, sasa anaanza kuifukuzia rekodi ya beki Mganda wa Simba SC, Juuko Murushid.
Serge Wawa yuko katika msimu wake wa pili Tanzania Bara akiwa amecheza mechi 56, lakini hajafunga hata bao la mkono |
Juuko aliye katika msimu wa pili pia Bara, hadi sasa amecheza mechi 41 na kufunga mabao mawili Msimbazi.
Tofauti ya Juuko na Wawa, walioanza mara moja kucheza baada ya kusajiliwa, Bossou alilazimika kusubiri hadi Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aumie Novemba mwaka jana ili kuanza kucheza.
Juuko Murushid (kulia) anawazidi Serge Wawa na Bossou idadi ya mabao ya kufunga Tanzania Bara |
Ilifikia wakati hadi waandishi na wachambuzi wa vyombo vya habari wakaanza kuamini Yanga SC imesajili mchezaji galasa, kutokana na Bossou kutopangwa – lakini baada ya kuanza kucheza amebadilisha upepo.
Sasa wana Yanga SC wanamkubali Bossou kama beki wa kazi ambaye anazimudu hata mechi zinazochafuka, kama ile dhidi ya Azam FC iliyotawaliwa na undava.
Sasa wana Yanga wanapenda Bossou apangwe kila mechi ngumu, baada ya shughuli alioionyesha ndani ya mechi 10 tu za mwanzo.
Bossou (kushoto) alilazimika kusugua sana benchi hadi Nadir Haroub 'Cannavaro' alipoumia Novemba |
0 comments:
Post a Comment