![]() |
Sinkala anajifaua na kikosi cha CHAN |
Mshambuliaji James Chamanga wa Liaoning Whowin ya China na kiungo wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Nathan Sinkala wameungana na kikosi cha wachezaji wa nyumbani watupu cha Chipolopolo katika kambi ya Lusaka tangu Desemba 21.
Kocha wa Zambia, Lusekelo Kamwambi milango iko wazi kwa wachezaji wote wanaocheza nje waliopo mapumzikoni kwa sasa kufanya mazoezi na kikosi cha CHAN ili wajiweke fiti kwa mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 Machi mwakani, ambapo Zambia itamenyana Kongo Brazzaville.
Zambia imepangwa Kundi D katika CHAN ya 2016 pamoja na Zimbabwe, Mali na Uganda na Chipolopolo wataanza na na mahasimu wao na jirani zao, Zimbabwe Januari 19.
0 comments:
Post a Comment