Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC wataingia kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani Jumatatu kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC watasafiri hadi Tanga Desemba 12, mwaka huu kuwafuata Mgambo JKT katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Jumatatu wanakwenda kambini kwa maandalizi zaidi ya mchezo huo.
Wachezaji wote waliokuwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge wamekwishajiunga na wenzao mazoezini, kasoro Haruna Niyonzima pekee.
Nahodha wa Rwanda ‘Amavubi’, Niyonzima ni kati ya wachezaji watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ambao leo watacheza fainali ya CECAFA Challenge.
Wengine ni beki wa Uganda na Simba SC, Juuko Murushid na kiungo wa Rwanda na Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza na wote wanatarajiwa kurejea kwenye klabu zao Jumatatu.
Pamoja na kuweka kambi Bagamoyo, Yanga SC itaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.

Niyonzima anatarajiwa kujiunga na wenzake kuanzia Jumatatu |
Nahodha wa Rwanda ‘Amavubi’, Niyonzima ni kati ya wachezaji watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ambao leo watacheza fainali ya CECAFA Challenge.
Wengine ni beki wa Uganda na Simba SC, Juuko Murushid na kiungo wa Rwanda na Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza na wote wanatarajiwa kurejea kwenye klabu zao Jumatatu.
Pamoja na kuweka kambi Bagamoyo, Yanga SC itaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment