// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YATAMBA KUBEBA POINTI ZOTE SITA MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YATAMBA KUBEBA POINTI ZOTE SITA MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 10, 2015

    YANGA SC YATAMBA KUBEBA POINTI ZOTE SITA MKWAKWANI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC ipo mjini Tanga tangu jana kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mgambo JKT na wamesema dhamira ni ushindi tu.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba kikosi kipo imara na tayari kabisa kwa mchezo wa Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani.
    “Tuko vizuri na tayari kabisa kuchukua pointi sita katika mechi zetu mbili mfululizo za Tanga,”amesema Muro na kuongeza; “Tunatambua itakuwa michezo migumu, lakini tumejipanga vizuri kwa ajili ya kushinda,”amesema.
    Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga SC

    Yanga itacheza na African Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, kabla ya kurudi tena kwenye Uwanja huo Jumatano kumenyana na ndugu zao, African Sports.
    Ikumbukwe Ligi Kuu ilisimama kwa takriban mwezi mzima kupisha mechi za timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria mwezi uliopita na baadaye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.
    Na wakati Ligi Kuu inasimama, Yanga SC ambao ndiyo mabingwa watetezi walikuwa katika nafasi ya pili kwa pointi zao 23, nyuma ya Azam FC iliyokuwa na pointi 25.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATAMBA KUBEBA POINTI ZOTE SITA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top