// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA KUANZA NA VIBONDE LIGI YA MABINGWA, WAKIWATOA WANAPEWA NA AL AHLY, AZAM WAPITA BILA JASHO RAUNDI YA AWALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA KUANZA NA VIBONDE LIGI YA MABINGWA, WAKIWATOA WANAPEWA NA AL AHLY, AZAM WAPITA BILA JASHO RAUNDI YA AWALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 12, 2015

    YANGA KUANZA NA VIBONDE LIGI YA MABINGWA, WAKIWATOA WANAPEWA NA AL AHLY, AZAM WAPITA BILA JASHO RAUNDI YA AWALI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Cercle de Joachim ya Mauritius katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati Azam FC itaanzia Raundi ya Kwanza.
    Azam FC itakutana na mshindi kati Bidvest Wits ya Afrika Kusini na wawakilishi wa Shelisheli amabo hawajapatikana.
    Yanga itaanzia nyumbani kati Februari 12, 13 na 14 mwakani huku ikimalizia ugenini kati ya Februari 26, 27 na 28 na ikivuka hatua hiyo, 
    itakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland.

    Na kama ikivuka tena hatua hiyo, itakutana na Al Ahly ya Misri, au mshindi kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Racing Micomiseng ya Equatorial Guinea.
    Azam FC itaanzia kucheza ugenini kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18, 19 na 20 na ikivuka mtihani huo, itakutana na ama Esperance ya Tunisia, wawakilishi wa Chad au News Stars de Douala ya Cameroon.
    Mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo wataanzia Raundi ya awali na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati JKU itacheza na Gaborone ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUANZA NA VIBONDE LIGI YA MABINGWA, WAKIWATOA WANAPEWA NA AL AHLY, AZAM WAPITA BILA JASHO RAUNDI YA AWALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top