KOCHA Mreno, Jose Mourinho amefukuzwa kazi Chelsea leo kwa mujibu wa shirika la Utangazaji Uingereza BBC.
Hiyo inafuatia mabingwa hao wa England, Chelsea kufungwa mechi tisa kati ya 16 za mwanzoni mwa msimu huu, wakiambulia pointi 15.
Mreno huyo alirejea Stamford Bridge mwaka 2013 na msimu uliopita akaiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

Kocha Mreno, Jose Mourinho amefukuzwa kazi Chelsea kutokana na matokeo mabaya |
Taarifa imethibitisha kwamba wameachana na Special One ingawa wamesema matokeo hayakuwa mazuri kiasi cha kutosha.
"Klabu ya soka ya Chelsea na Jose Mourinho leo wametengana maridhaino na heshima," imesema taarifa hiyo na hatua hiyo inakuja baada ya Chelsea kufungwa mabao 2-1 na Leicester katika Ligi Kuu ya England.
Guus Hiddink aliyeiongoza timu hiyo kwa muda mwaka 2009, anatarajiwa tena kuchukua nafasi ya Mourinho kwa muda kumalizia msimu na anaweza kuwepo kuiongoza timu katika mchezo dhidi ya Sunderland mwishoni mwa wiki hii.
Lakini pia Juande Ramos, Brendan Rodgers na Fabio Capello wote wanatakwa katika orodha ya wanaotarajiwa kurithi mikoba ya Mourinho kwa sasa, ingawa mpango wa muda mrefu ni klabu hiyo kumchukua Diego Simeone, ambaye atawagharimu Pauni Milioni 15 kuvunja Mkataba wake na Atletico Madrid.
Hii inakuwa mara ya pili Mourinho anafukuzwa Stamford Bridge kwa matokeo mabaya, baada ya awali kufukuzwa katika awamu yake ya kwanza ya kufundisha timu hiyo, mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment