KATIKA kujibu tetesi kuhusu Cristiano Ronaldo kuhusishwa na kuhamia klabu kadhaa miezi michache iliyopita, wakala wa Mwanasoka huyo Bora wa Dunia mara tatu, Jorge Mendes amesema kwamba Real Madrid itakuwa klabu yake ya mwisho kuchezea.
Tetesi zinasema mustakabali wa Ronaldo ndani ya Real unaelekea ukingoni, baada ya mtambo huo wa mabao kuripotiwa kumuambia Laurent Blanc kwamba angependa kucheza chini ya kocha huyo wa Paris Saint-Germain, huku gazeti la Le Parisien la Ufaransa likiandika: "Timu yako inacheza vizuri sana," baada ya Real kushinda 1-0 dhidi ya PSG kwenye Ligi ya Mabingwa mapema Novemba.
Lakini wakati Mendes akichukua tuzo Globe Soccer Jumapili mjini Dubai, aliweka wazi mteja atabaki La Liga na Real.
Cristiano Ronaldo ameweka picha hii katika ukurasa wake wa Instagram Jumapili akisema: "Narejea nyumbani baada ya awamu mbili'
"Ni mchezaji bora wa muda wote," Mendes amewaambia Sky Sports. "Na nina uhakika atacheza kwa miaka mingine minne, mitano, sita, saba akiwa Real Madrid; atamalizia soka yake huko. "Ana furaha na Los Blancos; atastaafu atakapofikisha umri wa miaka 40" amesema Mendes.
Ronaldo alifunga mabao mawili Real ikishinda 10-2 dhidi ya Rayo Vallecano Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumapili ya Desemba 20, kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwenda mapumziko Marekani wakati La Liga iliposimama kwa muda kupisha majira ya baridi.
Jorge Mendes amesema hayo baada ya kupokea tuzo 'Wakala wa Mwaka' mjini Dubai
0 comments:
Post a Comment