BONDIA Tyson Fury amevuliwa taji la ubingwa wa dunia wa IBF uzito wa juu, kiasi cha wiki mbili tangu alitwae.
Fury alimpiga bingwa wa muda mrefu, Wladimir Klitschko mjini Dusseldorf mwezi uliopita na kuyarejesha mataji yote manne ya bondia huyo wa Ukraine nchini Uingereza.
Lakini baada ya Klitschko kuchagua haki yake ya pambano la marudiano, IBF imemuondoa Fury kwenye orodha ya mabingwa wake.
IBF imesema Fury fight anatakiwa kupigana na mshindani wao mkuu wa uzito huo, Vyacheslav Glazkov na ikamtaka kutoa jibu ndani ya 48 baada ya ushindi wake bondia huyo mwenye umri wa miaka 27.
Fury alimpiga Wladimir Klitschko na kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu duniani katika pambano lililofanyika mjini Dusseldorf
Desemba 11 ilitarajiwa kuwa tarehe rasmi ya kutangaza pambano hilo, lakini imeshindikana baada ya Klitschko kusema atacheza pambano la marudiano mwakani.
Glazkov sasa atapambana na Charles Martin kuwania taji lililoachwa wazi la IBF - maana yake kipengele cha uzito wa juu katika ndondi ambacho kwa muda mrefu ubabe wake umekuwa unashikiliwa na Klitschko sasa kimeparaganyika.
Wakati Fury ataendelea kushikilia mataji ya WBO, WBA na IBO, Mmarekani Deontay Wilder ni bingwa wa WBC.
0 comments:
Post a Comment