WAWAKILISHI wa Afrika katika klabu bingwa ya dunia, TP Mazembe wataanza na mshindi kati ya wenyeji na Auckland City katika Robo Fainali ya michuano hiyo.
Bingwa wa Japan, wenyeji wa michuano hiyo ya FIFA mwaka huu bado hajapatikana na Gamba Osaka itamenyana na Sanfrecce Hiroshima katika mechi maalum ya kuamua bingwa kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha usajili wa wachezaji Desemba 7.
Mabingwa hao wa Afrika, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wanajivunia kikosi chao chenye wachezaji nyota kutoka nchi mbalimbali Afrika kama Roger Assale wa Ivory Coast, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wa Tanzania, Rainford Kalaba wa Zambia na kipa mkongwe wa DRC, Robert Kidiaba.
Mbwana Samatta ndiye tegemeo la mabao TP Mazembe kwa sasa
Tayari timu sita kati ya saba zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo katika miji ya Osaka na Yokohama nchini Japan zimewasilisha usajili wao makao makuu ya FIFA.
Wawakilishi wa Oceania, Auckland City, wanarejea katika Klabu Bingwa ya Dunia kwa mara ya saba baada ya kumaliza nafasi ya tatu mwaka jana nchini Morocco na watafungua dimba na wenyeji Desemba 10 kuwania kwenda Robo Fainali, ambako watakutana na Mazembe.
Club America itakutana na mabingwa wa Asia, Guangzhou Evergrande kwenye Robo Fainali ya Kwanza Desemba 13, wakati mabingwa wa Copa Libertadores, River Plate wataanzia Nusu Fainali Desemba 16 sawa na mabingwa wa Ulaya, Barcelona ambao watacheza Desemba 17.
(Gonga hapa kusoma vikosi vilivyowasilishwa kwa ajili ya Klabu Bingwa ya Dunia)

0 comments:
Post a Comment