// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TOC YAAGIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUSHIRIKIANA NA WANAMICHEZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TOC YAAGIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUSHIRIKIANA NA WANAMICHEZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 10, 2015

    TOC YAAGIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUSHIRIKIANA NA WANAMICHEZO

    Na Rahma Khamis na Miza Othman, ZANZIBAR
    KAMATI ya Olimpiki Tanzania  (TOC)  wamewataka Viongozi wa Mashirika ya  Vyama  vya Michezo  Tanzania  kusaidiana na wanamichezo mbalimbali ili kufikia hadhi ya kimataifa .
    Hayo yameelezwa na na Katibu mtendaji wa TOC Jamal Nassor Adi  huko Kituo cha Utengamano Welezo  Zanzibar wakati alipokua akifungua  Mkutano  mkuu wa mwaka wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania .
    Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhamasisha na kuamsha ari kwa Wachezaji ili kuweza kurejesha hadhi ya Michezo  Tanzania.
    Katibu Jamal amefahamisha kuwa wachezaji  ndio wahusika wakuu wa michezo hivyo ni lazima kushirikishwa na kupatiwa elimu ili kuweza kufahamu  wajibu wao katika michezo na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

    Mwenyekiti wa Kamisheni ya wachezaji Tanzania (KAWATA) Ramadhan Zimbwe akizungumza na Wanamichezo mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.


    Akizungumzia suala la dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo,  Katibu Jamal amesema  ni vyema wachezaji kuzifahamu na kujiepusha nazo kwani kitendo hicho kinaweza kupelekea nchi kupigwa marufuku kushiriki michezo ya Kimataifa.
    Naye Katibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania Filbert Bayi amesema kuwa michezo ni chanzo cha kujipatia  ajira  kwa vijana  hivyo ni vyema michezo  iendelezwe ili kuleta maendeleo kwa wachezaji wenyewe  na Taifa kwa ujumla.
    Aidha  amesema katika kuimarisha michezo Nchini   suala la kuteuliwa wawakilishi  wenye uwezo   ni jambo muhimu  na amewashauri washiriki wa mkutano  huo kusaidia ili kupunguza malalamiko.
    Mwenyekiti wa Kamsheni ya  Wachezaji Tanzania (KAWATA) Ramadhani Zimbwe ameahidi kupambana na rushwa kwa viongozi na watendaji  wa michezo nchini kwani  vitendo hivyo vinarudisha nyuma  ufanisi wa michezo.
    Amesema rushwa ni adui wa haki na mara nyingi hupelekea mtu mwenye uwezo wa kifedha kupata haki asiyostahiki na kumuacha mwenye haki hiyo kuikosa kutokana na kukosa fedha. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOC YAAGIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUSHIRIKIANA NA WANAMICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top