// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SUNDAY OLISEH ATAJA KIKOSI CHA SUPER EAGLES B KWA AJILI YA CHAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SUNDAY OLISEH ATAJA KIKOSI CHA SUPER EAGLES B KWA AJILI YA CHAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 08, 2015

    SUNDAY OLISEH ATAJA KIKOSI CHA SUPER EAGLES B KWA AJILI YA CHAN

    KOCHA wa Super Eagles, Sunday Oliseh amewaita Gbolahan Salami, Chima Akas na wengine 24 katika kikosi chake cha awali cha Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mapema mwakani nchini Rwanda.
    Kikosi cha Super Eagles B kimepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja na Niger, Tunisia na Guinea na kitacheza mechi zake Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
    Pia amewaorodhesha Kalu Orji, Austin Oboroakpo, Jamiu Alimi, Ifeanyi Mathew, Paul Onobi, Usman Mohammed, Bature Yaro, Ezekiel Bassey, Tunde Adeniji, Chisom Chikatara, Prince Aggrey, Ikechukwu Ezenwa na Olufemi Thomas.
    Sunday Oliseh (kulia) ametaja kikosi chake cha CHAN ya mwakani nchini Rwanda

    Wachezaji wote walioitwa kwenye kikosi cha Nigeria iliyoshinda Medali ya Shaba katika CHAN iliyopita nchini Afrika Kusini mwaka 2014, wameagizwa kuripoti kambini mjini Abuja Jumatatu ya Desemba 14.
    MIchuano hiyo ya nne inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, inatarajiwa kuanza Januari 16 hadi Februari 7, mwaka 2016.
    Kikosi kamili ni pamoja na makipa: Ikechukwu Ezenwa (Sunshine Stars), Olufemi Thomas (Enyimba), David Obiazor (Heartland), Okemute Odah (Warri Wolves)
    Mabeki: Kalu Orji (Enugu Rangers), Austin Oboroakpo (Warri Wolves), Jamiu Alimi (3SC), Mathew Etim (Enugu Rangers), Stephen Eze (Sunshine Stars), Chima Akas (Sharks), Chris Madaki (Giwa FC)
    Viungo: Ifeanyi Mathew (El-Kanemi Warriors), Paul Onobi (Sunshine Stars), Usman Mohammed (FC Taraba), Bature Yaro (Nasarawa United), Osas Okoro (Enugu Rangers), Bartholomew Ibenegbu (Warri Wolves), Julius Ubido (Heartland FC), Ibrahim Salawa Attah (3SC), Christian Madu (Enugu Rangers)
    Washambuliaji; Ezekiel Bassey (Enyimba FC), Gbolahan Salami (Warri Wolves), Tunde Adeniji (Sunshine Stars), Bright Onyedikachi (FC IfeanyiUbah), Chisom Chikatara (Abia Warriors), Prince Aggrey (Sunshine Stars).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUNDAY OLISEH ATAJA KIKOSI CHA SUPER EAGLES B KWA AJILI YA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top