// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STEPHEN KESHI ASHINDWA KUZUIA MACHOZI BAADA YA KIFO CHA MKEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STEPHEN KESHI ASHINDWA KUZUIA MACHOZI BAADA YA KIFO CHA MKEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 12, 2015

    STEPHEN KESHI ASHINDWA KUZUIA MACHOZI BAADA YA KIFO CHA MKEWE

    KOCHA na mchezaji wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi (pichani kulia) amesikitishwa mno na kifo cha mkewe kilichotokea Jumatano.
    Kate Keshi amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa miaka mitatu.
    Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria alishindwa kuzuia machozi yake wakati anaelezea kifo cha mkewe.
    "Nimepatwa na mshituko mkubwa. Alikuwa mgonjwa sana kwa muda mrefu, lakini hivi karibuni alianza kupata nafuu, hivyo hilo limekuwa pigo kubwa kwangu. Alikuwa rafiki yangu mzuri, hivyo huu ni mtihani mzito.
    “Nataka kumshukuru kila mmoja ambaye ametuma salamu zake za rambirambi katika familia,” amesema Keshi akizungumza supersport.com kutoka Marekani.
    Kate, aliyefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 54, aliolewa na Keshi miaka 33 iliyopita na wamefanikiwa kupata watoto wanne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEPHEN KESHI ASHINDWA KUZUIA MACHOZI BAADA YA KIFO CHA MKEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top