// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STAND UNITED YASAINI 'BEKI HALIPITIKI' KUTOKA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STAND UNITED YASAINI 'BEKI HALIPITIKI' KUTOKA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 02, 2015

    STAND UNITED YASAINI 'BEKI HALIPITIKI' KUTOKA IVORY COAST

    Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
    KILA klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania iko katika kuimarisha timu yake na jana Stand United ya mkoani Shinyanga ilifanikiwa kunasa saini ya beki kutoka Ivory coast, Assouman N'guessan David (pichani kushoto).
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, jana Msemaji wa timu hiyo, Deo Makomba alisema kuwa beki huyo amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Olympique Sports Abobo ya Ivory Coast.
    Makomba alisema kwamba uamuzi wa kusajili mchezaji huyo unatokana na mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo na wanaamini ujio wake utaimarisha safu ya ulinzi ya Stand United.
    'Haya ni mapendekezo ya kocha wetu, wakati huu wa dirisha dogo la usajili, lakini pia tupo mbioni kuwasana wachezaji wengine wawili wa hapa hapa nyumbani, " alisemama Makomba.
    Katika hatua nyingine, uongozi wa Stand United imewatoa kwa mkopo wachezaji wake watatu kwenda Polisi Tabora ambao ni Heri  Khalifa, Khalid Suleiman na Rashid Magona wakati Jisendi Mathias amepelekwa Geita Goldmine FC huku Hamad Ndikumana, Hamad Manzi, Shabani Dunia na John Mwenda wameachwa kuwa huru.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED YASAINI 'BEKI HALIPITIKI' KUTOKA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top