KLABU bingwa ya Ethiopia, St George imewasilisha barua katika klabu ya Azam FC kutaka kumnunua mshambuliaji chipukizi, Kevin Friday.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema St George imetuma barua rasmi ya kumwalika Friday akafanye majaribio ya wiki moja, ambayo akifuzu atasajiliwa.
"St. Georges inamtaka Kelvin Friday kwa majaribio ya wiki moja, imeshatutumia barua rasmi leo na sasa tunaifanyia kazi kwani ndio tumeipokea asubuhi hii, hivyo kwa baadaye tutajua anatakiwa kwenda huko lini baada ya kuwasiliana nao," alisema.
Friday ni mmoja ya wachezaji waliokulia kwenye Azam FC Academy na kupandishwa timu kubwa, moja ya sifa yake kubwa ni uwezo wa kupiga mashuti ya mbali.
St Georges hivi sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mholanzi Mart Nooij, ambaye amewahi kumuita mara kwa mara Friday kwenye kikosi cha Stars akianzia na Taifa Stars Maboresho.

Kevin Friday anatakiwa na St George ya Ethiopia |
Friday ni mmoja ya wachezaji waliokulia kwenye Azam FC Academy na kupandishwa timu kubwa, moja ya sifa yake kubwa ni uwezo wa kupiga mashuti ya mbali.
St Georges hivi sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mholanzi Mart Nooij, ambaye amewahi kumuita mara kwa mara Friday kwenye kikosi cha Stars akianzia na Taifa Stars Maboresho.
0 comments:
Post a Comment