Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imekamilisha usajili wa wachezaji wake wote iliyowaingiza katika dirisha dogo na inatarajiwa kuwatumia kesho katika mechi dhidi ya Azam FC, kasoro Brian Majwega.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba wametuma majina ya beki Novat Makunga, kiungo Brian Majwega na washambuliaji Paul Kiongera na Hajji Ugando Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Aidha, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema wamefanikiwa pia kupata leseni ya mshambuliaji Danny Lyanga, hivyo ataanza kucheza baada ya kukwama tangu mwanzo mwa msimu.
Majwega amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuvunja Mkataba wake na Azam FC, wakati Kiongera ni mchezaji wa Simba SC aliyekuwa anacheza kwa mkopo, KCB ya kwao, Kenya.
Makunga kutoka African Sports na Ugando kutoka Mtibwa Sugar B wote ni chipukizi ambao walikuwa wanacheza kama wachezaji wa ridhaa katika klabu zao.
Poppe amesema kwamba Hati ya Uhamisho wa Kimataifa ya Kiongera (ITC) tayari imefika, hivyo anaweza kucheza dhidi ya Azam FC kesho.
Hata hivyo, Poppe amesema Majwega atalazimika kusubiri kuanza kuitumikia Simba SC hadi klabu yake ya zamani, KCC ya kwao Uganda iridhie.
“Wakati Majwega anasaini Azam kutoka KCC, kulikuwa kuna makubaliano wakimuuza popote lazima KCC wapate mgawo. Sasa sisi huyu mchezaji Azam wametupa bure, KCC wanafikiri kuna biashara imefanyika, wameweka pingamizi,”amesema Poppe.
Lakini Poppe ameongeza kwamba Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajiwa kukutana kesho – pamoja na mambo mengine itajadili suala la Majwega.
“Ni matumaini yetu hakuna suala kubwa hapa. Ni jambo la kueleweshana tu na uzuri KCC wenyewe wanajua hali halisi kuhusu Majwega na Azam FC kwamba walikwishindwana, ndiyo maana imebidi aje kwetu,”amesema Poppe.

Brian Majwega atalazimika kusubiri KCC itoe ridhaa ili aanze kuitumikia Simba SC |

0 comments:
Post a Comment