// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAMSAJILI RASMI MAJWEGA NA BEKI LA AFRICAN SPORTS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAMSAJILI RASMI MAJWEGA NA BEKI LA AFRICAN SPORTS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 03, 2015

    SIMBA SC YAMSAJILI RASMI MAJWEGA NA BEKI LA AFRICAN SPORTS

    AZAM FC imekubalia kumuachia winga wake Mganda, Brian Majwega ajiunge na Simba SC.
    Ofisa Habari wa Simba SC, Hajji Manara amesema kwamba Majwega alionyesha dhahiri kupenda kuichezea Simba na hivyo ikaulazimu uongozi kumkabidhi kwa benchi la ufundi chini ya kocha wetu Dylan Kerr ili amfanyie tathimini.
    "Baada ya kupata ripoti kutoka katika benchi letu la ufundi kuwa kiwango cha Majwega kinaweza kusaidia kikosi cha Simba na kwakuwa mchezaji mwenyewe Majwega alionyesha nia ya kutaka kuichezea Simba, hivyo uongozi wa Simba na uongozi wa Azam FC ulikutana kujadili suala hili na mpaka sasa mazungumzo yanaonesha kuwa kwa asilimia kubwa mchezaji Brian Majegwa atachezea klabu ya Simba baada ya kufungwa kwa dirisha dogo,"amesema Manara.
    Brian Majwega sasa kuichezea Simba SC 

    "Ni imani yetu kuwa mazungumzo yatamalizika vizuri na mchezaji Majwega kuweza kwenda kwenye klabu ambayo anatamani kuichezea kwa sasa."ameongeza.
    Wakati huo huo: Simba imefanikiwa kumnasa beki wa kati wa African Sports ya Tanga, Novat Lufungo kwa dau la Sh, milioni 10.
    Tayari mchezaji huyo amekamilisha mazungumzo na ameshatua Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Azam utakaofanyika Desemba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Wekundu wa Msimbazi zinaeleza kuwa Lufungo ambaye aliwahi kuichezea Mgambo JKT kabla ya kujiunga na African Sports, amesaini mkataba wa miaka miwili.
    Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alithibitisha usajili wa beki huyo umekamilisha na tayari ni mchezaji halali wa klabu hiyo yenye makao mkuu Mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini.
    Naye Makamu Mwenyekiti wa African Sports, Abdul Bosnia aliliambia gazeti hili kuwa tayari Simba imefanikiwa kumnasa mchezaji huyo na wanamtakia kila la kheri katika majukumu yake mpya kwenye timu hiyo ya Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI RASMI MAJWEGA NA BEKI LA AFRICAN SPORTS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top