// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA YANGA ZAELEKEA ‘KUCHEMSHA’ USAJILI DIRISHA DOGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA YANGA ZAELEKEA ‘KUCHEMSHA’ USAJILI DIRISHA DOGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 08, 2015

    SIMBA NA YANGA ZAELEKEA ‘KUCHEMSHA’ USAJILI DIRISHA DOGO

    Na Waandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAKATI dirisha dogo la usajili linaelekea kufungwa Desemba 15, mwaka huu – vigogo Simba na Yanga SC wanaonekana kutofanikisha mawindo yao.
    Azam FC imeimarisha lango lake kwa kumsajili kipa mkongwe, Ivo Mapunda aliyewahi kudakia, Yanga SC, Simba SC, St George ya Ethiopia na Gor Mahia ya Kenya.
    Na kwa Muingereza Stewart John Hall mwenye kikosi kilichosheheni nyota wa aina tofauti, chipukizi wenye vipaji na wakongwe, kwake imetosha.
    Simba SC hadi sasa imesajili wachezaji wawili tu, Mganda Brian Majwega kutoka Azam FC kwa mkopo na Mkenya, Paul Kiongera ambaye ilikuwa ina Mkataba naye na alikuwa anacheza KCB ya kwao kwa mkopo.
    Michael Olunga yuko kwenye rada za Simba SC, lakini inaonekana klabu hiyo imekata tamaa ya kumpata

    Aidha, kuna makinda wengine wawili, beki Novat Makunga kutoka African Sports na mshambuliaji Hajji Ugando kutoka Mtibwa Sugar B wanajaribiwa na wanaonekana kuvutia katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo visiwani Zanzibar, lakini haipotezi ukweli kwamba hawakidhi mahitaji ya klabu kwa sasa.   
    Mara baada ya Ligi Kuu kusimama mwezi uliopita, kocha Muingereza Dylan Kerr aliwasilisha mapendekezo yake juu ya wachezaji anaotaka kuongeza kikosini na wengi aliwaona Azam na Yanga, lakini uongozi ukamuambia haua ubavu wa kuchukua nyota yoyote Chamazi wala Jangwani.
    Makubaliano yakawa kutafutwa wachezaji wengine wenye viwango vya nyota aliowatamani kutoka Azam na Yanga ambao ni pamoja na mabeki wa kati wawili, winga na mshambuliaji.
    Labda mshambuliaji ni Kiongera baada ya kukosekana Mrundi Laudit Mavugo na Mkenya Michael Olunga waliokuwa wanatakiwa, na winga ni Majwega – lakini kwa beki ya kati Simba inaonekana imekwama na siku zinayoyoma.
    Kwa upande wao, Yanga SC japokuwa wanaonekana wana kikosi kilichosheheni wachezaji mahiri, lakini kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm alitaka kuongeza wachezaji wawili na kuondoa mmoja.
    Issoofou Garba kutoka Sierra Leone anatakiwa na Yanga SC

    Dhamira ya Pluijm ni kupata beki wa kushoto na mshambuliaji na akaushauri uongozi kusitisha Mkataba wa kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho ili kuongeza nafasi ya kusajili wachezaji wa kigeni.
    Na Pluijm inadaiwa ndiye aliyependekeza kuletwa kwa kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar Garba.
    Popote katika wasifu wake, Garba mwenye umri wa miaka 26 anatambulishwa kama kiungo – lakini Yanga wanasema wanaleta mshambuliaji.
    Na huyu atakuwa mchezaji wa pili kuletwa na kocha Pluijm, baada ya awali kumleta beki Joseph Zuttah ambaye hata hivyo aliachwa baada ya mechi saba.
    Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
    Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 
    ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
    Wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.
    Lakini pia, kwa Yanga kuna tetesi za kutaka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Elias Maguri ambaye kwa sasa anacheza Stand United.
    Bado wapenzi na mashabiki wa soka nchini, hususan manazi wa timu hiyo wanaendelea kufuatilia kwenye vyombo mbalimbali vya habari kujua klabu hizo zitafanya nini katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZAELEKEA ‘KUCHEMSHA’ USAJILI DIRISHA DOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top