// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA AZAM BONGE LA MECHI YANGA WATAKUWA MKWAKWANI AKILI ZIPO TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA AZAM BONGE LA MECHI YANGA WATAKUWA MKWAKWANI AKILI ZIPO TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 11, 2015

    SIMBA NA AZAM BONGE LA MECHI YANGA WATAKUWA MKWAKWANI AKILI ZIPO TAIFA

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA…
    Desemba 12, 2915
    Kagera Sugar vs Ndanda FC
    Stand United vs Mwadui FC
    Mbeya City vs Mtibwa Sugar
    Azam FC vs Simba SC
    Majimaji vs Toto Africans
    Mgambo JKT vs Yanga SC
    Desemba 13, 2015
    JKT Ruvu vs Prisons
    Coastal Union vs African Sports
    Desemba 16, 2015
    African Sports vs Yanga SC
    Desemba 19, 2015
    Yanga Africans vs Stand United
    Mwadui FC vs Ndanda FC
    Kagera Sugar vs African Sports
    Prisons vs Mtibwa Sugar
    Toto Africans vs Simba SC
    Majimaji vs Azam FC
    Desemba 20, 2015
    JKT Ruvu vs Coastal Union
    Mbeya City vs Mgambo JKT
    Desemba 23, 2015
    Azam FC vs Mtibwa Sugar
    Desemba 26, 2015
    Ndanda FC vs JKT Ruvu
    Yanga SC vs Mbeya City
    Paul Kiongera amerejea Simba SC na anatarajiwa kucheza kesho dhidi ya Azam FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inarejea kesho baada ya mapumziko ya takriban mwezi mzima kupisha mechi za timu ya taifa na michuano ya Kombe la CECAFA Challenge.
    Nyasi za viwanja sita zitawaka moto kesho, lakini macho na masikio ya wengi vitaelekezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambako vigogo Simba SC watakuwa wanamenyana na Azam FC.
    Azam FC wanahitaji ushindi katika mchezo wa kesho kujiimarisha kileleni na kuzidi kuwaacha mabingwa watetezi, Yanga SC wakati Simba SC inahitaji ushindi ili kurudi kwenye mbio za ubingwa.
    Na hapo ndipo ulipolalia utamu na msisimko wa mchezo huo, kiasi kwamba hata mashabiki wa Yanga ingawa timu yao itakuwa Uwanja wa Mkwakwani kesho ikimenyana na Mgambo JKT, lakini watakuwa wanasikilizia kinachoendelea Taifa.
    Na sana Yanga SC wanaitakia ushindi Simba SC au hata sare, ili mahasimu wao hao, Azam FC katika mbio za ubingwa wapunguzwe kasi. 
    Simba SC imeimarisha kikosi chake katika dirisha dogo kwa kumrejesha mshambuliaji wake Mkenya, Paul Kiongera aliyekuwa anacheza kwa mkopo KCB ya kwao.
    Ivo Mapunda aliyeiyumikia Simba SC miaka miwili iliyopita, amesajiliwa Azam FC, je kesho atadaka?

    Aidha, Wekundu hao wa Msimbazi pia wamesajili chipukizi wawili, beki wa kati Novat Makunga kutoka African Sports ya Tanga na mshambuliaji Hajji Ugando kutoka Mtibwa Sugar B, ingawa haijulikani kama watakamilishiwa utaratibu wa kupata leseni kabla ya mechi za kesho.
    Azam FC yenyewe imemsajili kipa mkongwe, Ivo Mapunda aliyewahi kudakia Yanga SC, Tukuyu Stars, Prisons, Moro United, African Loyon, Simba za Tanzania pia na St George ya Ethiopia na Gor Mahia ya Kenya.
    Mabingwa watetezi, Yanga SC wao kesho watakuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kumenyana na timu ngumu, MGambo JKT ya Kabuku, Tanga.  
    Mechi nyingine za ligi hiyo kesho; Kagera Sugar wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Stand United wakiongozwa na kinara wa mabao Ligi Kuu, Elias Maguri wataikaribisha Mwadui FC, Mbeya City wataikaribisha Mtibwa Sugar, Majimaji wataikaribisha Toto Africans, wakati Jumapili JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Karume na Coastal Union watamenyana na mahasimu wao, African Sports.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA AZAM BONGE LA MECHI YANGA WATAKUWA MKWAKWANI AKILI ZIPO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top