WAKATI natumia kurasa zangu za Facebook, Instagram na Twitter kumpigia debe mgombea Urais wa CCM, Dk John Pombe Joseph Magufuli nilipata shida kidogo.
Wafuasi wangu walinikasirikia na wengine wakatishia hadi kutonifuatilia tena. Wengine tulifarakana wakati huo, kwa sababu hawakutumia maneno ya busara.
Siyo tu kwa sababu waliichoka CCM kiasi hicho, bali wengi walimuunga mkono zaidi mgombea wa Ukawa na Chadema, Edward Lowassa.
Katika umri wangu huu takriban miaka 40 ninamjua Lowassa na ninamjua pia Magufuli – lakini niliona nchi hii kwa sasa inamuhitaji Yule ambaye nilikuwa nawaomba Watanzania wenzangu wamchague.
Jana katimiza mwezi mmoja madarakani tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini si hapa nchini tu, bali Magufuli amekuwa gumzo dunia nzima.
Watanzania wote sasa wanamkubali Magufuli, kwa sababu amekuja kufanya kazi ambayo wanaipenda na ninaamini na ninatarajia mengi.
Ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma, ukwepaji kodi wa kiasi kikubwa, ubadhirifu wa mali za umma, rushwa, wizi, ufisadi vyote vinatarajiwa kukoma kabisa katika Serikali ya awamu ya tano.
Watu kujiona wao ni ‘Miungu Watu’ kiasi kwamba wanaweza kunyanyasa wengine na wala wasiguswe. Dhuluma ya mali za masikini. Unyanyasaji wa wananchi wa hali ya chini wanaobangaiza kupata kiasi kidogo cha mboga na unga navyo vitakoma.
Watanzania sasa wana matumaini ya kweli ya kuishi kwa amani na furaha katika nchi yao.
Na ninaamini, baada ya miaka yake mitano ya kwanza, Magufuli hatahitaji matamasha ya Clouds Entertainment katika kampeni zake, kitu ambacho ni ufujaji mwingine wa fedha.
Tunamshukuru Rais aliyemaliza muda wake, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutufikisha hapa na tunamtakia kila la heri Rais mpya, Dk Magufuli.
Baada ya yote aliyoyafanya ndani ya mwezi mmoja wa kuwa kwake madarakani, watu sasa wanasubiri zaidi kusikia Baraza lake la Mawaziri.
Watu wanataka kujua ataunda Baraza la Mawaziri wangapi. Litakuwa na Mawaziri wa aina gani.
Kwa sisi wanamichezo ndiyo tuna kiu haswa ya kujua Wizara yetu itakuwa chini ya akina nani.
Huku kwenye michezo ndiyo kumeoza kabisa. Kurugenzi yote ya Michezo ovyo. Mawaziri wa Michezo wa siku za karibuni wamekuwa watu wa kuhudhuria shughuli kama wageni rasmi, lakini hawana cha ziada walichoifanyia sekta hiyo.
Kamati ya Olimpiki Tanzania (BOT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), idara za Utamaduni na Sanaa, kote huko kumeoza na ndiyo maana michezo nchini imeporomoka.
Kwa kiasi kikubwa sasa tunategemea Majeshi yetu ya ulinzi na Usalama tu kutuzalishia wanamichezo ambao ndiyo wanatumika kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa, lakini hakuna chochote.
Katika sanaa sasa tunajua Bongo Fleva na Bongo Muvi tu, zaidi ya hapo tumeua kabisa sanaa na utamaduni wa asili ambao ndiyo ungeweza kututambulisha zaidi kama taifa.
Misafara ya timu zetu kwenye michezo ya kimataifa kama Michezo ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Olimpiki imekuwa na viongozi wengi kuliko wachezaji.
Mfumo mzima wa kuibua na kuwaendeleza wanamichezo nchini kwa sasa umekuwa ovyo na kisingizio chao kikubwa imekuwa eti kufa kwa michezo mashuleni.
Ukiwauliza wao walifanya jitihada gani kipindi hicho katika kuibua vipaji, kuviendeleza na hatimaye baadaye wawe na wanamichezo hodari wa kuunda timu bora za taifa usitarajie jibu la maana zaidi ya blablah!
Vyama vya michezo, ukiondoa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) vyote havina vyanzo vya mapato na kwa bahati mbaya aina ya viongozi ambao vimekuwa vikipata siku za karibuni wameshindwa kuvikwamua kiuchumi.
Na kwa sababu nchi hii sasa imechafula, Mameneja Masoko wa makampuni mengi wanaidhinisha udhamini baada ya kujihakikishia watanufaika na wao.
Ndiyo maana kuna vitu vya ovyo visivyo hata na mvuto wa kijamii, lakini makampuni yanawekeza fedha nyingi, ila hayako tayari kusaidia michezo au wanamichezo ambao kwa dhati wangesaidia umaarufu wa bidhaa zao.
Tanzania tuna vinywaji vingi vya kuongeza mwilini, lakini ni kipi kinadhamini michezo ya nguvu jamii ya ndondi?
Kwa sababu hii si ajabu michezo imekufa Tanzania. Hakuna msisimko tena wa ndondi, kikapu, Riadha, Mieleka na hata hiyo soka yenyewe inabebwa na unazi wa Simba na Yanga tu.
Tunahitaji Wizara mpya ya Michezo itakayokuja kushughulika michezo kwa dhati kabisa, kwanza kubadilisha kabisa mfumo wa kiuatawala na ufundi – lakini pia kujihusisha na maendeleo ya michezo kiukamilifu.
Hatuhitaji Waziri ambaye atasubiri kuambiwa njoo uzindue mashindano, njoo ukabidhi Kombe au njoo uwe mgeni rasmi katika usiku wa sherehe za tuzo.
Tunahitaji Waziri ambaye atashirikiana na Watendaji wa Wizara yake kufanya shughuli za maendeleo ya michezo, ambayo imekufa kwa sasa Tanzania.
Tunahitaji Waziri ambaye ataisafisha Kurugenzi ya Michezo, TOC na BMT.
Tunahitaji Waziri ambaye atasaidia kurejesha wataalamu wengi wa michezo kama waliokuwapo enzi za Mwalimu Julius Nyerere (sasa marehemu), Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, Marais wa awamu tatu za mwanzo.
Tunahitaji Waziri ambaye hatawaogopa TFF, CAF wala FIFA katika kupambana kwa ajili ya maendeleo ya soka ya Tanzania.
TFF wamejiwekea kinga kutoka FIFA, kwamba wao hata wafanye madudu vipi, hawawezi kuwajibishwa na dola – lakini wanasahau kwamba wanaitegemea Serikali ili kufanikisha ndoto za kuinua mchezo wao, unaoongoza kupendwa nchini.
Ni wakati sasa, TFF chini ya Rais mweledi tu, Jamal Malinzi iwe tayari kushirikiana bega kwa bega na Serikali kama ambavyo nchi nyingine zilizoendelea zinafanya.
Malinzi peke yake bila msaada wa Serikali hawezi kupambana na wizi na ubadhirifu unaofanywa ndani ya TFF, ambao yeye anaweza tu kuhisi upo, lakini asijue watu wanaibaje na wakati gani.
Nchi za Magharibi, Nigeria kwa mfano mara ngapi Serikali imekuwa ikifukuza viongozi wa Shirikisho la Soka baada ya kujiridhisha wameboronga? Ndiyo maana wenzetu wanakwenda Kombe la Dunia. Wanakuwa mabingwa wa Afrika. Wana wachezaji wa kulipwa Ulaya.
Sasa na sisi tunahitaji mabadiliko katika sekta ya michezo Tanzania na tunaamini hayo yatawezekana iwapo Dk Magufuli atatupatia Waziri safi.
Sifa za Waziri safi ni zile zile alizotumia kumpata Waziri Mkuu wake Majaliwa– lazima asiwe mpenda sifa na umaarufu, awe hana kashfa za ufisadi na awe mzalendo kweli, zaidi awe anaijuajua michezo japo kidogo ili asije kudanganywa.
Tunahitaji mabadiliko katika sekta nzima ya michezo. Imeoza.

0 comments:
Post a Comment