Huyu ndiye Rais wa Chama cha Soka Sierra Leone, Isha Johansen
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeifungulia Sierra Leone kuandaa tena michuano ya shirikisho lake.
Katika barua ya Desemba 6, 2015, iliyosainiwa na Katibu wa CAF, Hicham El Amrani na kuelekezwa kwa Rais wa Chama cha Soka Sierra Leone (SFA), Isha Johansen, nchi hiyo imefunguliwa.
Sasa maana yake mecho zote za mashindano ya CAF kuanzia za klabu na kimataifa zitachezwa katika nchi hiyo ya Magharibi mkwa Afrika, baada ya kusimama tangu Agosti 2014 baada ya CAF kutii agizo la Shirika la Afya Duniani (WHO) kuzuia mechi za soka kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Nchi nyingine zilizohusika na agizo hilo ni Guinea, Liberia na Sierra Leone, lakini kwa sasa ni Guinea pekee ambayo haijafunguliwa kutokana na WHO kutothibitisha kutoweka kwa ugonjwa huo nchini humo.

0 comments:
Post a Comment