MABINGWA wa Afrika, TP Mazembe wamepoteza ndoto za kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia, baada ya mchana wa leo kufungwa mabao 3-0 na Sanfrecce Hiroshima katika mchezo wa Robo Fainali Uwanja wa Nagai mjini Osaka.
Kwa ushindi huo, Sanfrecce itakutana na River Plate ya Argentina katika Nusu Fainali Desemba 16, wakati Mazembe itamenyana na Club America siku hiyo kuwania nafasi ya tano Uwanja wa Nagai.
Mabao ya wenyeji hao yamefungwa na Tsukasa Shiotan dakika ya 44, Kazuhiko Chiba dakika ya 56 na Takuma Asano dakika ya 78.
Kazuhiko Chiba (katikati) akishangilia baada ya kuifungia Sanfrecce bao la pili leo
Mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mbwana Samatta alicheza kwa dakika zote 90, wakati Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu aliingia mwanzoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzambia, Given Singuluma.
Mchezo wa kwanza, Guangzhou Evergrande ya China imeifunga America ya Mexico mabao 2-1 na sasa itakutana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona katika Nusu Fainali Desemba 17.
Mechi ya kusaka mshindi wa tatu na fainali zinatarajiwa kuchezwa Desemba 20.

0 comments:
Post a Comment