// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SANFRECCE YAING'OA AUCKLAND CITY...KUIVAA TP MAZEMBE JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SANFRECCE YAING'OA AUCKLAND CITY...KUIVAA TP MAZEMBE JUMAPILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 11, 2015

    SANFRECCE YAING'OA AUCKLAND CITY...KUIVAA TP MAZEMBE JUMAPILI

    MABAO ya Yusuke Minagawa na Tsukasa Shiotani jana Uwanja wa Kimataifa wa Yokohama, yametosha kuipeleka Sanfrecce Hiroshima Robo Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya kuilaza Auckland City 2-0.
    Sanfrecce, wakitoka kutwaa ubingwa wa Ligi ya Japan Jumamosi, J.League walistahili ushindi wa jana dhidi ya mabingwa wa Oceania. 
    Kikois cha Hajime Moriyasu sasa kitamenyana na mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Jumapili katika Robo Fainali mjini Osaka na mshindi wa mchezo huo, atamenyana na River Plate ya Argentina Desemba 16 Uwanja wa Nagai mjini Osaka katika Nusu Fainali.

    Wachezaji wa Sanfrecce Hiroshima wakishangilia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Auckland City jana

    Club America ya Mexico Jumapili itamenyana na Guangzhou Evergrande ya China na mshindi atakutana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona Desemba 17 Uwanja wa Yokohama katika Nusu Fainali.
    Mechi za kusaka mshindi wa tatu na fainali zitachezwa Desemba 20 Yokohama. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SANFRECCE YAING'OA AUCKLAND CITY...KUIVAA TP MAZEMBE JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top