// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA: DILI LA ULAYA LIMEKAA POA, NASUBIRI WAKATI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA: DILI LA ULAYA LIMEKAA POA, NASUBIRI WAKATI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 13, 2015

    SAMATTA: DILI LA ULAYA LIMEKAA POA, NASUBIRI WAKATI TU

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WAKATI leo anatarajiwa kuiongoza timu yake, TP Mazembe katika mchezo wa Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema safari ya Ulaya imeiva.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwa simu kutoka Osaka, Japan jana ambako yuko na TP Mazembe kwa ajili ya Kombe la Dunia, Samatta amesema mipango ya kuhamia Ulaya imekamilika.
    “Mipango imefikia katika hatua za mwisho, ila naweza kusema mambo yanakwenda vizuri na wakati ukifika nitasema timu gani ninakwenda,”amesema Samatta.
    Mbwana Samatta (kulia) akiwa na 'patna' wake Thomas Ulimwengu

    Samatta na Mtanzania mwenzake, Thomas Emmanuel Ulimwengu leo wanatarajiwa kuiongoza Mazembe katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji, Sanfrecce Hiroshima.
    Wakati Mazembe imeanzia moja kwa moja Robo fainali, wenyeji hao walilazimika kuitoa Auckland City kwa kuifunga 2-0, mabao ya Yusuke Minagawa na Tsukasa Shiotani katika mchezo wa mchujo.
    Mshindi kati ya kikosi hicho cha Hajime Moriyasu na Mazembe mjini Osaka leo, atamenyana na River Plate ya Argentina Desemba 16 Uwanja wa Nagai mjini Osaka katika Nusu Fainali.
    Mchezo mwingine leo utazikutanisha Club America ya Mexico na Guangzhou Evergrande ya China na mshindi atakutana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona Desemba 17 Uwanja wa Yokohama katika Nusu Fainali.
    Mechi za kusaka mshindi wa tatu na fainali zitachezwa Desemba 20 Yokohama.
    Samatta, aliyezaliwa Januari 7, mweaka 1992 alijiunga na Mazembe mwaka 2011 akitokea Simba SC, ambayo aliichezea kwa msimu mmoja tu baada ya kuhama African Lyon.
    Hadi sasa ‘Sama Goal’ ameifungia Mazembe mabao 60 katika mechi 103 za mashindano yote.
    Mdogo huyo wa kiungo wa Mgambo JKT, Mohammed Samatta mwaka jana alikwenda kufanya majaribio CSKA Moscow ya Urusi, ambako bahati mbaya akaumia baada ya siku tatu na kurejea Lubumbashi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA: DILI LA ULAYA LIMEKAA POA, NASUBIRI WAKATI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top