// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SABA WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI LA WACHEZAJI WA THE CRANES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SABA WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI LA WACHEZAJI WA THE CRANES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 08, 2015

    SABA WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI LA WACHEZAJI WA THE CRANES

    WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, The Cranes wamepata ajali iliyosababisha vifo vya watu saba jana.
    Wachezaji wa The Cranes walikuwa wanatoka wilaya ya Soroti baada ya kukutana na Rais Yoweri Museveni walipoalikwa baada ya kutwaa taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini Ethiopia Jumapili.
    Ajali hiyo ilisababishwa na tairi la mbele la basi lililokuwa limebeba wachezaji wa Cranes kupata pancha na kupoteza mwelekeo eneo la Mbale katika maegesho ya teksi ya Jami mjini Kamonkoli, wilaya ya Budaka.
    Basi la The Cranes likiwa limegongana na basi dogo la abiria


    Kikosi cha The Cranes kikikuwa na Rais Museveni kabla ya kwenda kupata ajali

    Basi hilo la The Cranes lilikwenda kuigonga gari ndogo ya abiria (Hiece) na kusababisha vifo vya watu saba, kwanza watatu wakifariki papo hapo.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) imesema wachezaji watatu Kezironi Kizito, Denis Okot Oola, Hassan Wasswa Dazo na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya FUFA, Ahmed Hussein wameumia.
    Ofisa wa Usalama barabarani wa Bukedi, Paul Okongo amewataja baadhi waathirika wa ajali hiyo kuwa ni Charles Mwima, Wahab Nakifuyi, Zainabu Nabusuyi na Samuel Kagulu, wakati wengine hawajatambulika. 
    "Dereva wa basi la The Cranes ndiye anastahili lawama kwa ajali hii, kwa sababu alikuwa anaendesha kwa kasi sana," amesema Okongo. “Alishindwa kulimudu gari baada ta tairi moja kupasuka,"
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SABA WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI LA WACHEZAJI WA THE CRANES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top