Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba amekwishamuondoa kiungo Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima katika mipango yake na sasa anasonga mbele bila yeye.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo mjini Dar es Salaam, Pluijm amesema kwamba anaunga mkono hatua iliyochukuliwa na uongozi, kwa sababu Haruna ameshindwa kujiheshimu kama mchezaji wa kulipwa.
Pluijm amesema kwamba sasa anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na amekwishamfuta Haruna katika daftari lake la wachezaji.
Yanga SC jana imevunja Mkataba na kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda kwa madai ya mchezaji huyo wa Amavubi kukiuka vipengele.
Na Pluijm anakuwa mtu mwingine muhimu ndani ya Yanga SC kuunga mkono adhabu hiyo, baada ya Milionea Abdallah Ahmed Bin Kleb aliyemleta Niyonzima Jangwani.
“Mimi kwa kweli ninaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na uongozi, kwa sababu suala la nidhamu ni la muhimu mno katika timu. Kama mchezaji ameshindwa kuheshimu Mkataba wake, hii ni hatua sahihi,”alisema Bin Kleb jioni ya jana.
Aidha, Bin Kleb ambaye alisajili nyota wengine kadhaa Yanga SC akiwemo kiraka Mbuyu Twite, amewataka wapenzi na wanachama wa klabu kuunga mkono uamuzi wa uongozi.
“Unajua Haruna ni mchezaji mwenye kipaji, ambaye ana wapenzi wengi pale Yanga SC, ambao najua hawataufurahia uamuzi huu. Lakini mimi napenda nichukue fursa hii kuwaomba wana Yanga wote tuungane na uongozi kuafiki hatua hii,”.
“Mchezaji kama ameshindwa kuheshimu thamani aliyopewa ndani ya klabu, wazi huyo hafai. Haruna tulimchukua kwa Mkataba wa miaka miwili awali, baadaye tukamuongeza miwili. Ikaisha na juzi ametoka kuongezewa mwingine wa miaka miwili,”.
“Sasa nadhani amekwishajiona mwenyeji kwenye timu anafanya anavyotaka bila kuzingatia Mkataba wake unasemaje. Ni sahihi tu hatua iliyochukuliwa,”amesema Kleb.
Aidha, Bin Kleb alisema anaamini hatua iliyochukuliwa itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine, ili waweze kuheshimu mikataba yao wakati wote.
Sakata la kufukuzwa kwa Niyonzima Yanga SC, linaanzia mwezi uliopita baada ya mchezaji huyo kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Challenge nchini Ethiopia na akachelewa kurejea baada ya mashindano.
Kufuatia hali hiyo, klabu ilimsimamisha kwa muda usiojulikana Niyonzima kabla ya suala lake kupelekwa Kamati ya Nidhamu, ambayo hatimaye imekuja na maamuzi magumu.
Pamoja na Niyonzima kuwasilisha vielelezo vyote vya kumsafisha, lakini uchunguzi wa Kamati ya Nidhamu ulijiaminisha kiungo huyo amedanganya ili kukwepa hatua za kinidhamu.
Ulibaini plasta gumu (PoP) alilofunga baada ya kurejea akiwa amechelewa ilikuwa ni ‘geresha’ na vielelezo vingine alivyowasilisha vilikuwa ‘feki’ pia.
Na ikamnasa kwenye picha za video siku za karibuni ‘akijirusha’ sehemu mbalimbali za starehe ikiwemo kwenye onyesho la mwanamuziki Ali Kiba.
Haruna aliyezaliwa Februari 5, mwaka 1990 Gisenyi nchini Rwanda, alijiunga na Yanga SC mwaka 2011 akitokea APR ya kwao, ambako aliwasili mwaka 2007 akitokea Rayon aliyoichezea kwa misimu miwili baada ya kujiunga nayo akitokea Etincelles iliyomuibua mwaka 2005.

Haruna Niyonzima alikuwa kipenzi cha Pluijm kabla ya matatizo haya |

0 comments:
Post a Comment