Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amependekeza jina la mshambuliaji hatari kutoka Afrika Magharibi na sasa uongozi wa klabu upo katika mchakato wa kumleta nchini.
Yanga SC imevunja Mkataba na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho na sasa ina nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kigeni ili kutimiza saba tena kwa mujibu wa kanuni.
Pluijm anataka kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji na tayari jina la mpachika mabao kutoka Magharibi mwa Afrika lipo mezani kwa Katibu Mkuu, Dk. Jonas Tiboroha ambaye kwa sasa yupo nchini Ghana.
Ingawa Pluijm aliwahi kuleta beki Mghana, Joseph Zuttah ambaye aliachwa baada ya kucheza mechi saba tu, lakini uongozi wa Yanga SC umeamua kumpa nafasi nyingine Mholanzi huyo.
Bado jina la mchezaji huyo na nchi anayotoka linafanywa siri kubwa na wote kati ya viongozi wa Yanga SC, ingawa inatarajiwa atatokea Ghana kwa sababu ni nchi ambayo Pluijm alifanya kazi kabla ya kuja Tanzania.
Wachezaji wa kigeni ndani ya Yanga SC kwa sasa ni mabeki Mbuyu Twite kutoka DRC, Vincent Bossou wa Togo, viungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, Thabani Kamusoko, washambuliaji Donald Ngoma wa Zimbabwe na Amissi Tambwe wa Burundi.
Pamoja na kwamba Pluijm ana washambuliaji wazawa pia kikosini akina Malimi Busungu na Matheo Anthony Simon, lakini bado anahitaji mshambuliaji mmoja zaidi wa kigeni.
Yanga SC ambayo mwakani itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika inataka kuwa na kikosi imara kabla ya michuano hiyo ya CAF.

Kocha Hans van der Pluijm analeta mshambuliaji hatari Yanga SC kutoka Afrika Magharibi |

0 comments:
Post a Comment