// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PLUIJM ‘AKUNWA’ NA MCHEZAJI WA NIGER BAADA YA KUMJARIBU KWA SIKU MBILI TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PLUIJM ‘AKUNWA’ NA MCHEZAJI WA NIGER BAADA YA KUMJARIBU KWA SIKU MBILI TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 11, 2015

    PLUIJM ‘AKUNWA’ NA MCHEZAJI WA NIGER BAADA YA KUMJARIBU KWA SIKU MBILI TANGA

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    KOCHA wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ameonekana kuvutiwa na kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar Garba baada ya mazoezi ya siku mbili na timu hiyo tangu awasili kwa majaribio.
    Yanga SC iliyoweka kambi katika hoteli ya Kwetu mjini Tanga kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana imefanya mazoezi Uwanja wa sekondari ya Galanosi, wakati leo asubuhi ilikuwa Mkwakwani. Na Garba ameshiriki kikamilifu mazoezi yote hayo kiasi cha kumvutia uwanjani kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
    Garba akifanya mazoezi mbele ya kocha Pluijm leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
    Pluijm ambaye anatakiwa kuamua kuhusu mchezaji huyo wa zamani wa Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia kabla ya kufungwa pazi la dirisha dogo la usajili Desemba 15, alionekana kufurahia kila mchezaji huyo alipokuwa na mpira.
    Na leo asubuhi katika mazoezi ya kupiga mikwaju ya penalti, Pluijm alifurahia Garba alipofunga kiufundi. 
    Garba aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1990, popote katika wasifu wake, anatambulishwa kama kiungo – lakini Yanga wanasema wameleta mshambuliaji.
    Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
    Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
    Wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.
    Yanga SC wakijifua Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo tayari kuwakabili Mgambo kesho
    Garba katikati akinyoosha viungo katika mazoezi leo asubuhi Uwanja wa Mkwakwani
    Garba akijiandaa kupiga penalti leo Uwanja wa Mkwakwani

    Katika mchezo wa kesho, Yanga SC inatarajiwa kuwakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza, akiwemo Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni majeruhi. 
    Wengine ni beki Oscar Joshua na viungo Haruna Niyonzima ambaye yuko kwao Rwanda na Salum Telela ambaye ni mgonjwa.
    Kuna wasiwasi Yanga pia ikamkosa mshambuliaji tegemeo lake la mabao kwa sasa, Donald Ngoma ambaye ameshindwa kufanya mazoezi na timu mjini Tanga kwa sababu ya maumivu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM ‘AKUNWA’ NA MCHEZAJI WA NIGER BAADA YA KUMJARIBU KWA SIKU MBILI TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top