// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIGO MAN UNITED, SCHWEINSTEIGER AFUNGIWA MECHI TATU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIGO MAN UNITED, SCHWEINSTEIGER AFUNGIWA MECHI TATU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 10, 2015

    PIGO MAN UNITED, SCHWEINSTEIGER AFUNGIWA MECHI TATU ENGLAND

    KIUNGO Bastian Schweinsteiger amefungiwa mechi tatu na Chama cha Soka England baada ya kugombana na Winston Reid wakati Manchester United ikitoa sare na West Ham.
    Uamuzi huo umefikiwa mbele ya jopo la marefa watatu ambao kila mmoja alirudia kutazama video ya tukio hilo ili kujionea vizuri kilichotokea.

    Bastian Schweinsteiger amefungiwa mechi tatu kwa kumpiga usoni mchezaji wa West Ham, Winston Reid PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Tukio hilo lilitokea kabla ya mapumziko, baada ya Schweinsteiger kumpiga usoni Reid wakati wanasubiri mpira wa kona. 
    Refa Mark Clattenburg alizungumza na wachezaji wote baada ya ugomvi huo, lakini hakuwachukulia hatua yoyote. 
    Pamoja na hayo, baada ya kubainika Clattenburg hakuona tukio hilo, FA ikamfungulia mashitaka Schweinsteiger Jumatatu.
    Baadaye Reid akasema nyota huyo wa Ujerumani alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu. "Anafahamu alichokifanya – alinipiga usoni. Refa hakuona, hivyo tunasonga mbele".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO MAN UNITED, SCHWEINSTEIGER AFUNGIWA MECHI TATU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top