MABAO mawili ya kiungo Etebo Peter Oghenekaro yameipa Nigeria ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 23 Afrika, kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Algeria katika fainali usiku wa jana Uwanja wa Leopold Sedar Senghor mjini Dakar, Senegal.
Mchezaji huyo wa Warri Wolves ya nyumbani, Nigeria alifunga mabao hayo kipindi cha kwanza wakati Oduduwa Segun alijifunga kuwapatia bao Algeria.
Algeria walipoteza nafasi ya kufunga bao la kusawazisha kwa penalti mwishoni mwa kipindi cha pili, baada ya kipa wa Nigeria, Emmanuel Daniel kuzuia mchomo wa Zinedine Ferhat.
Kocha wa Nigeria, Samson Siasia aliwastaajabisha wengi kwa kumuanzisha nyota wa Kombe la Dunia la FIFA la U-17, Victor Osimhen katika safu ya ushambulaji, naye akalipa fadhila kwa kuisaidia timu kupata penalti dakika ya 13 baada ya kuchezwa rafu na Nahodha wa Algeria, Ryad Keniche.
Oghenekaro akaenda kufunga kuipa timu hiyo ya Magharibi mwa Afrika bao la kuongoza la mapema.
dakika moja baadaye, kipa wa Algeria, Abdelkadir Salhi akaokoa mchomo wa hatari wa Oghenekaro kabla ya ‘Les Fennecs’ kusawazisha baada ya Oduduwa kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Ferhat.
Dakika tano kabla ya mapumziko, Oghenekaro akaifungia Nigeria bao la ushindi akimtungua Salhi na kufikisha mabao matano katika mashindano hayo.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Afrika Kusini waliwafunga wenyeji, Senegal kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 0-0.

Wachezaji wa Nigeria wakiwa na Kombe la ubingwa wa U-23 Afrika baada ya kukabidhiwa jana mjini Dakar |
Kocha wa Nigeria, Samson Siasia aliwastaajabisha wengi kwa kumuanzisha nyota wa Kombe la Dunia la FIFA la U-17, Victor Osimhen katika safu ya ushambulaji, naye akalipa fadhila kwa kuisaidia timu kupata penalti dakika ya 13 baada ya kuchezwa rafu na Nahodha wa Algeria, Ryad Keniche.
Oghenekaro akaenda kufunga kuipa timu hiyo ya Magharibi mwa Afrika bao la kuongoza la mapema.
dakika moja baadaye, kipa wa Algeria, Abdelkadir Salhi akaokoa mchomo wa hatari wa Oghenekaro kabla ya ‘Les Fennecs’ kusawazisha baada ya Oduduwa kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Ferhat.
Dakika tano kabla ya mapumziko, Oghenekaro akaifungia Nigeria bao la ushindi akimtungua Salhi na kufikisha mabao matano katika mashindano hayo.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Afrika Kusini waliwafunga wenyeji, Senegal kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 0-0.
0 comments:
Post a Comment