// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NI UGANDA KUBEBA TAJI LA 14, AU RWANDA KUNYAKUA LA PILI LEO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NI UGANDA KUBEBA TAJI LA 14, AU RWANDA KUNYAKUA LA PILI LEO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 05, 2015

    NI UGANDA KUBEBA TAJI LA 14, AU RWANDA KUNYAKUA LA PILI LEO?

    UGANDA, The Cranes leo watakuwa wanawania taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge watakapomenyana na Rwanda ‘Amavubi’ nchini Ethiopia.
    Michuano ya 38 ya CECAFA Challenge inafikia tamati leo mjini Addis Ababa kwa michezo miwili, kwanza wa kusaka mshindi wa tatu kati ya wenyeji, Ethiopia dhidi ya Sudan na baadaye Uganda na Rwanda.
    Korongo wa Kampala walio chini ya kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ndiyo mabingwa wa kihistoria wa CECAFA Challenge wakiwa wamebeba taji hilo mara 13 katika miaka ya 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009, 2011 na 2012.
    Uganda walitwaa taji hilo kwa mara ya mwisho nyumbani mwaka 2012

    Rwanda imetwaa taji hilo mara moja tu mwaka 1999, lakini leo wanacheza fainali ya tano zikiwemo zile za 1990, 1996 na 2013.
    Micho atakutana na timu ambayo miaka mitatu iliyopita alikuwa anaifundisha na anaijua vizuri Amavubi na wachezaji wake- jambo ambalo linatarajiwa kuwa kipaumbele kwake kufanya vizuri leo.
    Lakini shaka tu ni kwamba Rwanda hii ya kocha Muingereza, Johnny McKinstry ina mbinu tofauti na wachezaji wake wanajimudu ipasavyo kiushindani uwanjani.
    Uganda inashika nafasi ya 68 katika viwango vya ubora wa soka duniani, wakati Rwanda ni ya 96. Hadi kufika hapa, kila timu imepoteza mechi moja tu na zote za makundi, Rwanda ilifungwa 2-1 na Tanzania Bara na Uganda ilifungwa 2-0 na Kenya.
    Uganda ilifuzu kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Malawi katika Robo Fainali kabla ya kuwatoa wenyeji Ethiopia kwa matuta, wakati Rwanda imekuwa ikifuzu kwa matuta kuanzia Robo Fainali ikiwatoa mabingwa watetezi, Kenya na Nusu Fainali ikiwang’oa Sudan.
    Nani kuwa bingwa wa 38 wa CECAFA Challenge leo? Ni Rwanda kutwaa taji la pili, au Uganda kubeba la 14? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI UGANDA KUBEBA TAJI LA 14, AU RWANDA KUNYAKUA LA PILI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top